Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Denis Mpagaze
__________________________
Leo kila mtu analia maisha magumu. Ukimuuliza ni magumu kivipi, atakwambia anadaiwa ada ya mtoto, anadiwa kodi, mke ana matumizi mabaya.
Unapeleka mtoto shule ya gharama kubwa kuliko kipato chako ili wakuone unazo!
Mwingine kapeleka watoto wake shule za gharama kwa sababu mke wake kamwambia afanye hivyo waonekane wa kishua.
Huu ni ufahari mzuri wenye matokeo mabaya. Maisha lazima yakupeleke. Ukicheza unakwenda na maji.
Ukiishi kulingana na urefu wa kamba yako maisha hayasumbui sana.
Uwezo wako ni kula utumbo wa kuku, gonga huo huku ukiendelea kuzitafuta, ipo siku utakula kuku mzima na utumbo utatupa!
Mwingine ametumia kahela kake kote kununua simu ya gharama, wanaita Aifoni sree ili tu wamuone. Sasa sijui wakimuona anapata nini!
Haya wamekuona. Kwahiyo? Ona unakosa hata bando la buku jero kwenye simu ya milioni. Mizinga ya vocha inakushusha sana.
Mwingine kachukua mkopo kanunua gari na wakati uwezo wa kiwese hana, siku amekosa kiwese naye anasema maisha magumu. Kweli?
Mwingine kapanga nyumba ya gharama ya juu zaidi ya kipato chake, mwenye nyumba akija kudai anasema maisha ni magumu, amvumilie.
Kwani ukipanga kule kwenye sogea tukae hadi utakapopata pesa za kutosha kuishi kwenye nyumba nzuri utakufa?
Maisha siyo magumu sisi ndiyo wagumu. Tunajitwisha mizigo kuliko uwezo wetu.
Mwingine amezima simu siku nzima, michepuko yake inamsumbua, inataka kodi ya nyumba na hela ya kusuka.
Huyu naye ukikutana atanasema maisha ni magumu. Onaona tunavyojichanganya?
Unashindwa kuhudumia visivyo vya lazima halafu unasema maisha ni magumu. We vepee?
Umekopa vikoba kununua vitu usivyovihitaji ili kuwarusha roho wasiokupenda. Haya umewarusha sawa. Kwahiyo?
Unajua shida nyingine tunajiletea wenyewe na kurusha lawama kwa maisha.
Fanya majaribio ya kuishi kulingana na urefu wa kamba yako hata kwa mwezi mmoja uone kama hujafurahia maisha.
Haya maisha ni rahisi sana. Ukiacha mikogo utaenjoy sana. Kuendelea kujali vitu vinavyokuzidi uwezo utaumia. Utakosa raha yakhe!