Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
James na Jamila walianza mapenzi wakiwa shule ya upili. Walipofika kidato cha tatu Jamila alipata ujauzito, ilibidi aache shule. James alendelea kidato cha tano na sita.
Jamila alijifungua mtoto wa kike mzuri na kumpa jina Aisha. James alitoka shuleni anamkuta Jamila na mtoto, alipenda kumsaidia lakini mwenyewe alitegemea msaada wa wazazi wake.
Jamila alifanya I biashara vya hapa na pale na katika kuhaika na malezi alijikuta anaingia katika mahusiano mengine. Alipata ujauzito wa pili, mwanaume aliahidi kumhudumia. Walianza maisha pamoja.
James alipata nafasi ya kwenda chuo kusomea uhandisi. Huku kwa Jamila baba wa mtoto alimfahamisha kuwa ametafutiwa mchumba nyumbani kwao anakwenda kuingia kwenye ndoa. Jamila aliachwa na watoto wawili sasa bila baba.
Maisha yaliendelea, Jamila aliuza uji, alipika maandazi na maisha yalikua yale ya kupika ugali mboga ni fungu la samaki wa 1,000. Ugali matembele, ugali mchicha.
James alituma pesa alipoweza, pesa zo ikifika zilisaidia watoto kupata nguo za shule pamoja na za kuvaa nyumbani. James alifika kumuona Aisha kila alipopata nafasi. Siku James akifika menu nyumbani huwa ni ya heshima. Watoto wanakula wali na kuku hata na matunda baada ya chakula.
Mpaka James anamaliza chuo na kupata kazi, Jamila alikua na watoto wanne na kila mtoto na baba yake. James alipoweka mazingira vizuri alianza kumchukua Aisha wakati wa likizo. Ilikua shida kuanza kumfundisha Aisha taratibu na muda wa kulala, mambo ambayo hajazoea, kwa mama yake una lala pale unapochoka.
James alianza kumfundisha Aisha maneno ya Kiingereza, kumsomea vitabu nk. Likizo ilipokwisha wote wawili walitokwa na machozi, hakuna aliyetaka kumuacha mwenzake.
James alipata mchumba na kufunga ndoa. Alifanya taratibu zote za kumchukua Aisha na kuishi nae. Mke wa James alimpenda Aisha na maisha yaliendelea.
Aisha alimuona mama yake wakati likizo, Akifika kwa mama maisha ni yale ya mtoto kutumwa na bakuli asubuhi akalete maandazi. Sukari mnanunua kwenye kikombe ya kutosha leo tu.
Aisha alibahatika kuwa msomi pekee katika familia ya mama yake. Akitafakari anasema, isingekua kuishi na baba yake asingefika mbali kwani mazingira aliyoishi mama yake hayakuwapa wadogo zake nafasi ya kufika mbali.