Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Usijidanganye kwenda bondeni kutafuta maisha kama huna msingi, wala kibali. Kama unaweza kulipa nyumba Milioni kwa mwezi hapa Tanzania basi unaweza kuishi huko.

Kama unaweza kuishi Masaki na Mbezi beach basi unaweza kuishi huko sababu tabia za huko mazoea ya uswahilini hakuna, ukiweza kuishi South Africa na ndio umeweza kuishi nchi yoyote iliyopo Ulaya na pengine.

South Africa gredi ya uhalifu ni kubwa sana, kesi za kufa watu zipo nyingi kuliko kesi nyengine, ingekuwa tz kila siku kamanda wa polisi anatangaza mwisho hata choka.

Ngono kule ni kitu cha kawaida yani unatongoza mchana usiku unapewa, sio huku kwetu mpaka uchunwe kwanza.

Ukiwa na misosi ya kutosha na nyumba utachagua wanawake mpaka UKIMWI ukufikie, wanathamini kula sana maana maisha magumu kwao. Wezi, wauza madawa, wakwepa kodi na n.k wanaogopa kuweka pesa zao benki sababu benki za huku ni kama TRA kukuchunguza, Rais Ramaphosa ni mfano tosha.

Wizi wa magari ni kama wizi wa simu, gari nyingi zinazoingia hapa kwetu nyingi za wizi zinatoka huko. Vigogo wakubwa na wauza ngada hapa Tz wanaishi huko au kuwa na makazi ni wengi tu.

Msidanganye na wasanii wanasema wamenunua nyumba bali kule nyumba unaweza kununu tena nzuri ila ni kama umekodi, tofauti ya tanzania ardhi ina bei utadhani unanunua madini.

Kuvamiwa ni jambo la kawaida, wezi wakule usumbufu hawataki unaenda kwa order ukileta ubishi ni kugusa kaburini.

Huwezi kuchezea simu ovyo maana mitaa yote kuna wahalifu usipo kuwa makini unaweza kuona benzi kali inapita kumbe wapo wezi, ukifika nyumbani kama kuna geti lazima uchunguze mbele na nyuma nani anakufata ijalishi gari au mtembea miguu na hatua kidogo kabla ujafika getini, unaingia nao.

Vijana wetu waliozamia ukiona kaenda karudi katoboa maisha, mawili ni mchomoko au madawa.

Mchomoko ni kuvizia nyumba wenyewe hawapo tena nyumba hizi kama nilivosema wanaoweka pesa za kutakatisha.

South sio poa.
 
Nimeona kwenye clip kadhaa mtandaoni Wezi wanafika kuiba kwenye nyumba wakiwa kwenye Gari ya kifahari.

Na huwa ni either wanateka Gari la Mtu au kuingia na kuiba kwenye Nyumba ya Mtu huku wakionekana kwenye cctv.

Wakati mwingine hata Gari waliyokuja nayo ni kali kuliko ile wanayoiiba/iteka.
 
Nishazika washkaji wawili na mmoja alikuwa kama uncle wangu walikuwa huko south ila madogo hawa wengi mtaani hamna mtu wako uko yaani wako zaidi ya miaka 4 ila hWana kitu zaidi ya kushare nguo na kupost Instagram na fb.

Kuna wachache wakubwa walirudi miaka ya 2005 mpaka 2010 walikuwa na mitaji sasa wanaishi bongo na biashara zao..

Uchungu mmoja alirudi kawa teja kabisa sema kitaa walimlea sana mwaka 2017 katikati alichomwa moto mtaa wa jirani aliiba.

Wapo mabrodas wako huko wananiambia dogo usije ukaja huko sisi kwenye game tuko zaidi ya miaka 20 ila ngoma bado bila bila wanaona hata aibu kurudi bongo kuanza upya ila kimtindo wanasaidia wazazi wao maana washashusha hiace kadhaa zinakula vichwa town ,na Yale maboma ya wazazi wao washayakarabati ni nyumba safi ila bado Maisha ya kusave wnaaona ni Soo zaidi familia hawana wamezaa na madanga kila kona.
 
Umesahau na rape, hii kule wahalifu wanaona ni kawaida kubaka. South carjacking, house robbery, murder and rape ujitayarishe navyo. Sehemu salama kwako, labda uende sehemu za utalii. Kidogo huko polisi wanapalinda sana.

Sababu ya crime kuwa juu, South Africa. Wanasema baadhi tu ni Unemployment, Ufisadi mkubwa wa Serikali, hawajali tabaka la chini na Alcohol.
 
Umesahau na rape, hii kule wahalifu wanaona ni kawaida kubaka.
South carjacking, house robbery, murder and rape ujitayarishe navyo.
Sehemu salama kwako, labda uende sehemu za utalii. Kidogo huko polisi wanapalinda sana.

Sababu ya crime kuwa juu, South Africa. Wanasema baadhi tu ni Unemployment, Ufisadi mkubwa wa Serikali, hawajali tabaka la chini na Alcohol.
Pia wazawa awapendi Kazi zaidi ya pombe na ngono na hivi havipatikani bure.
South african hawana tofauti na black american wote Wana characters moja.
 
Pia wazawa awapendi Kazi zaidi ya pombe na ngono na hivi havipatikani bure.
South african hawana tofauti na black american wote Wana characters moja.
Yes wavivu, sasa wakienda Wazimbabwe na mataifa mengine ya Kiafrika, kufanya kazi. Ndiyo huanzishaga zile vurugu, kuwa wameenda kuwachukulia kazi zao.
 
Back
Top Bottom