Brazameni ni mwaka kamili tangu tukuone JF mara ya mwisho kabla ya leo.
Vipi hali yako? Karibu tena.
Tofauti za Egypt na Dubai:
Cairo ni mji mkubwa na wakizamani, Dubai ni mji mdogo sana (ukilinganisha na Cairo).
Egypt inaendesha na wa Egypt wenyewe katika kila nyanja, Dubai ni wageni kutoka nchi tofauti duniani. Kwa hiyo Dubai ni multi cultured city na Egypt ni mono cultured city.
Egypt ni wajanja wa maneno na utapeli, they can do anything to get the money except harm you physically. Ujanja huo Dubai hakuna.
Polisi na watu wa usalama wa Egypt ni washenzi sana (wakati wa Mubarak, sidhani kama wamebadilika) na sheria mkononi wanaweza wa kaku harass bila ya sababu. Wa Egypt hawapendi sana wageni.
Dubai hakuna harassment na usalama ni wali ya juu na wanaoishi Dubai wengi ni wageni, kwa hiyo ukifika hujulikani kama mgeni.
Dubai gharama za maisha kama nyumba, social, entertainment zipo juu sana kulinganisha na Egypt. Egypt ni uwezo wako, unaweza kuishi uoendavyo kikawaida kwa gharama ndogo au kifahari kwa gharama kubwa.
Cairo ni mji mzuri wa kuishi ikiwa una kazi yako nzuri na inakulipa vizuri lakini sio mji ambao unakwenda kutafuta kazi. Ni mji ambapo uende tayari una kazi za kufanya. Dubai unaweza kwenda kutafuta kazi.
Population ya Cairo ni kubwa sana na watu ni wengi sana kwa hiyo tegemea foleni za magari za hali ya juu kwa. Kelele za honi na watu haziepukiki baadhi ya sehemu (kwingi).
Kwa uchache, Dubai na Cairo (Egypt) ni vitu viwili tofauti.