Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,234
wanajamvi wenzangu,
Habari za jioni.
Kumekuwa na shida sana ya kupata na kuishi na hawa beki 3. Ni muhimu sana kwa maisha ya familia.
Familia yangu inahangaika sana. watoto bado wadogo, maisha magumu lazima tufanye kazi ili kuweza kusukuma gurudumu mbele.
Kama hiyo haitoshi, beki 3 wa siku hizi wamekuwa hatari sana, wengine wanawafanyia watoto mambo mabaya sana, wengine ni wachawi, mradi ni shida na mkanganyiko kwenye maisha ya familia. wazazi tunahangaika, watoto wanatabika. kazini hakukaliki, basi ni shida tupu.
Wenzetu, unafanyaje?
Mnapataje hawa beki 3?
toka kuanzishwa kwa shule za kata
huwezi pata housegirl kama zamani.....
unless uwe tayari kuwalipa better ....na sasa mshahara wao nasikia unaanzia elfu sitini....
ukitaka fanya kama wahindi wa city centre dar...
wanawalipa vizuri but hawalali majumbani
wanakuja na kuondoka na jumapili hawaji......na ukiwataka
unamuuliza housegirl yeyote wa wahindi city centre atakuletea.....
Ni rahisi kuwapata, but kuwapata ambao hawatakuwa na tabia ulizoorodhesha hapo juu ni kazi kweli kweli. Labda cha kukushauri, tafuta mtu unayemfahamu if possible toka kijijini kwako/mkeo, be careful na tabia zake na ikibidi mchukue akiwa na akili zake timamu. Mimi nilimchukua aliyezalishwa na kutelekezwa. Anajua machungu ya maisha na pia anajua kulea watoto, im happy.
Duh siku hizi ni balaa mkuu
Wasichana wameerevuka hata kule ambako kulikuwa wanasema wanapatikana imekuwa issue sana
Shule za kata nazo zinawaondoa kwenye ufanyakazi wa nyumbani na kwenda kusoma
hawataki tena kufanya kazi za nyumbani
Ni balaa sana kwa sasa
siku hizi taabu tupu,
hata uwape nini hawaridhiki...
Tena wengine wanafanya mambo ya ajabu ukisikia unabaki mdomo wazi?
Ila wapo wachache wametulia....
Lakini kama mama ni makini...
Yupo karibu na watoto
anasimamia nyumba kwa hali ya juu...
Kidogo inasaidia......
Na usiombe upate hg mwenye agenda mbili mbili......
Lazima amtege faza house.......................
toka kuanzishwa kwa shule za kata
huwezi pata housegirl kama zamani.....
unless uwe tayari kuwalipa better ....na sasa mshahara wao nasikia unaanzia elfu sitini....
ukitaka fanya kama wahindi wa city centre dar...
wanawalipa vizuri but hawalali majumbani
wanakuja na kuondoka na jumapili hawaji......na ukiwataka
unamuuliza housegirl yeyote wa wahindi city centre atakuletea.....