Maisha ya kila siku huku kwetu Kwamtogole

Maisha ya kila siku huku kwetu Kwamtogole

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mwenye saloon ya kusukia nywele anakodisha chumba. Ndani anaweka Drayer 2, vioo, microwave viti, kabati la display. Chini kuna carpet la blastic.

Sijakosea saloon kuna microwave, msusi anakuwa na cooler. Ukienda kusuka rasta saa ya kula anakuuliza utapenda pilau, ndizi nyama au wali maharage. Vyote hivyo vinakuwa frozen na vimwekwa kwenye kula. Ukisema pilau, inatolewa, inapashwa moto unapewa ni sh 3, 500.

Kabati la display lina hereni za rusha roho. Rusha roho ni mabati yaliyopakwa rangi ya dhahabu. Zinaitwa rusha roho kwani tunawarusha roho wavaa dhahabu 😂.

Hapo hapo kuna vikopo vya is mkorogo na vitenge. Vitenge unaweza kukopeshwa wakijua unafanya kazi gani au kama wewe ni mke wa pedeshee kama Asprin.

Mwenye saloon anaingiza pesa kwa biashara 4/5 katika chumba kimoja.
 
Dah...nasikiaga eti kwenye saluni za kike huwa kuna chumba cha kupumzika... nimesikia tu

Sent using Beretta ARX 160
 
Back
Top Bottom