Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 700
Kama destiny ya Elizabeth Michael na Cyntoia Brown zinafanana.
Hakuna stori mpya kwenye kesi inayomkabili msanii wa maigizo Elizabeth Michael, zaidi ya duwa na sala zetu usiku na mchana katika kumwombea msichana huyu ili ikiwezekana anusurike dhidi ya mkono wa sheria.
Swali kubwa ambalo mashabiki wote wa filamu hapa nchi wanajiuliza, Je nini itakuwa hatma ya msanii huyu baada ya kushtakiwa upya kwa kosa la kuua bila kukusudia?
Makala hii inafanya upembuzi wa kina na utafiti yakinifu dhidi ya kesi inayogusa hisia za watu kwa namna tofauti tofauti. Ili kupata majibu mahususi tutatizama kesi inayomkabiri Elizabeth Michael tukilinganisha na kesi iliyotikisa ulimwengu mwaka 2006, kesi iliyomuhusu muuaji wa miaka 16 raia wa Marekani anayejulikana kama Cyntoia Brown.
Mwaka 2004 Cyntoia Brown alikamatwa kwa kesi ya mauaji. Kulikuwa hakuna shaka yoyote kuwa Johnny Allen(43) alikuwa ameuwawa, na Cyntoia Brown ndiye aliyekuwa amefanya mauaji hayo.
Kama tunavyoona kwenye kesi ya Lulu, upande wa mashtaka ulishupalia kumtia hatiani Binti huyo mdogo bila kujali vigezo na mazingira yote yaliyokuwa yakidhihirisha kuwa Cyntoia Brown hakuwa na hatia.
Hii ni kesi pekee iliyovuma kimataifa na inayofanana kabisa na kesi ya Elizabeth Michael. Cyntoia Brown Alikuwa na Uhusiano wa kimapenzi na hayati John Allen kama ilivyokuwa kwa Elizabeth Michael na Marehemu Steven Kanumba.
Cyntoia Brown alifanya mauaji akiwa na umri wa chini ya miaka 18(mtoto) kama ilivyokuwa kwa Elizabeth michael. Cyntoia Brown alifanya kosa akiwa anajitetea asidhuliwe kama ilivyokuwa kwa Elizabeth Michael.
Cyntoia Brown alikuwa akiishi na mzazi mmoja tu wa kike kama ilivyo kwa Elizabeth Michael. Kesi ya Syntoia Brown ilichukua miaka miwili kabla ya hukumu, kama itakavyokuwa kwa Elizabeth Michael.
Baada ya Kuchunguza kwa makini utagundua kuwa Historia ya maisha ya Elizabeth Michael inafanana kabisa na historia ya Cyntoia Brown, Sanjari na historia za maisha, Hata mazingira ambayo Syntoia alifanya mauaji yaliyomtia hatiani ni mazingira yale yale yaliyomtia hatiani Elizabeth.
Je hatma ya mabinti hawa wawili inaweza kulingana?
Baada ya kesi ya Cyntoia kusota kwa miaka miwili tangia mwaka 2004, hatimae mwaka 2006 Cyntoia Brown alihukumiwa kifungo cha maisha. Huu ukawa muendelezo wa upofu katika sheria, unyanyasaji wa kwa watoto pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Katika kuhusisha wasifu wa Elizabeth Michal na Cyntoia Brown, mwaka 2010 tukio lisilokuwa la kawaida lilifanyika kwa lengo la kumuokoa Cyntoia kutoka katika hukumu ya uonevu na kusimamisha vita ya kimataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.
Muandaaji wa filamu Daniel Birman alifanya utafiti mkubwa kudhihirisha ni jinsi gani unyanyasaji kwa watoto umekuwa kitu cha kawaida, na nini kifanyike ili kupambana na taatizo hilo.
Alishangazwa sana kuwa inawezekanaje mtoto aliyelelewa katika maadili na matunzo mazuri maisha yake yawe na mwisho mbaya kiasi hiki. Hii ikampelekea Daniel Birman apeleleze historia ya maisha ya Cyntoia kwa zaidi ya miaka 6 na kuandaa documentary iliyopewa jina la Me Facing Life.
Jicho la kamera ya Bwana Daniel Birman lilimwangazia Cyntoia tangia wiki ya kwanza ya kukamatwa kwake mpaka mwaka 2010. Bila malengo ya kutaka kumtetea wala kumshuhudia Cyntoia kama mfano wa kizazi kilichoharibika, Daniel Birman alimfatilia Cyntoia Brown Kwa Muda wa miaka 6 tangia kukamatwa kwake.
Daniel Birman aliongozana bega kwa bega na bingwa mpelelezi wa matatizo ya kisaikolojia anaetambulika kitaifa nchini Marekani Dk William Bernet kutoka Chuo Kikuu cha Vanderbilt.
Kwa msaada na ushirikiano mkubwa wa mama mzazi Georgina Mitchell na Mama mlezi Ellenette Brown, tatizo kubwa liligundulika kuanzia kwenye malezi ya Cyntoya na life style ya maisha yake kabla ya kukamatwa na polisi.
Unyanyasaji mkubwa kwa Cyntoia ulianza mapema sana mara baada ya kuingizwa kwenye vitendo vya ngono akiwa na umri wa chini ya miaka 13 na kuanza kuishi na mwanaume mwenye miaka 24 ambaye alikuwa muuzaji na mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Cyntoia Alilazimishwa kufanya kazi ya kujiuza ili apate pesa ya kulipia kodi na kusaidia maisha yake na mwanaume huyo. Baada ya Maisha kuwa magumu zaidi, Cyntoia aliamua kumtoroka mwanaume huyo.
"Nilikuwa sijielewi, sijui ninakokimbia wala ninapokimbilia" ni kauli inayotolewa na Cyntoia sasa. Cyntoia anaendelea kusema, "Jamii ya Neville ilinipa maisha niliyokuwa nikidhani ni ya uhuru kumbe ulikuwa ni unyanyasaji na ukatili kwangu".
Makala hii inaamini kuwa Elizabeth michael na Syntoia Brown historia zao zitafanana mpaka mwisho, mpaka jamii atakapoamua kuchukua hatua za makusudi kumnusuru Lulu kutoka katika hukumu batili inayoweza kufanywa na mahakama.
Je, unyanyasaji ambao Cyntoya alifanyiwa na kumuathili kisaikolojia tangia akiwa na miaka 13 ulijitokeza kwa Lulu!? Ungana nami katika toleo lijalo ili uweze kusikia taarifa za uchunguzi madhubuti juu ya maisha ya Lulu tangia akiwa na miaka 13. Hapa hapa JamiiForum.
Documentary hii inautafiti pekee unaoweza kutumika kumsaidia Lulu kwenye kesi yake. Kama unasapoti utafiti huu like hii article ili nimalizie. Support huu uchunguzi tafadhali ili Jamiiforum tujenge historia ya uasisi wa vita vya kufa na kupona dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.
Wasomaji wangu wote wa the second Door tutaendelea na Ile kitu naombeni mwazo katika makala hii tafadhari.
g click, Kongosho, Heaven Sent, Ennie, Daudi1, everlenk, jembe afrika, HARUFU, mahirtwahir, Kasonso S., prospa, Payer, Phenomenon Lady, Mfagio, beth, Mwadunda, anna bubelwa, ram, dreadnaughty, Obe, wangewange, Luno G,Mrembo by Nature, Gunda66, Lolipop, Blaki Womani, Giti, Khantwe, Kyenju, Kaunga, Ennie, toghocho, twin'sisy, Arnooy1206, Mbimbinho, Meljons,davidson689, xfactor, kifagio.