Maisha ya msanii Hawa ni darasa tosha

kibla matata

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2020
Posts
412
Reaction score
380
Msanii hawa aliyefahamika zaidi kupitia wimbo wa Diamond Plutinumz wa Nitarejea. Aliwahi kukiri kwamba stress za maisha zilimpelekea kuingia katika maisha ya utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na utumiaji wa pombe kali, bange na pombe za kienyeji (mataputapu)

Hiyo ikapelekea kuuchukia wimbo wa nitarejea na kumlalamikia Diamond kwamba hakulipwa chochote kwenye wimbo wa Nitarejea.

Kutokana na utumiaji wa pombe kali ikapelekea kuugua ugonjwa wa ini na kujaa sana kwa tumbo. Diamond akamsaidia kumpeleka India kwa ajili ya matibabu na akapona. Sasa hivi anaendelea na muziki.

Ameachia wimbo mpya unaitwa Moyo ni wimbo mzuri; una maadili unaweza kuuangalia hata ukiwa na familia yako.

Hii inatufundisha jinsi gani Mungu anatoa another chance Kwa ajli ya kujirekebisha. Sasa hivi Hawa anaoga, anapendeza.

Kwa kifupi anajua kuimba. Simsifii sana.

 
Ungeweka na kawimbo tukaskie/tuone
 
Amejifundisha nini kuhusu alipomlaumu Diamond kua hakulipwa chochote kwenye wimbo wa nitarejea kisha huyo huyo Diamond ndio akampeleka India kutibiwa?

Sasa alikosea nini kusema ukweli kwamba hakulipwa? au ulitaka mwandishi akimuuliza ajibu ndio amelipwa ili ionekane hajalaumu India amekuja kupelekwa baadae
 
Daah! Huyu dada alikua na full stress, alifunga ndoa na jamaa mmoja hapo tabata kwa bibi walikua wanakaa sasa wakaachana kwa ugomvi sana naona jamaa akimuona sasa atahaibika
 
Daah! Huyu dada alikua na full stress, alifunga ndoa na jamaa mmoja hapo tabata kwa bibi walikua wanakaa sasa wakaachana kwa ugomvi sana naona jamaa akimuona sasa atahaibika
Hilo ni funzo kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…