Shida Masuba
Member
- May 30, 2016
- 6
- 4
MAISHA YA MTANZANIA KIUCHUMI TANGU MWAKA 2021-
Maisha ni jumla ya mambo yanayokuzunguka na uyafanyayo kila iitwapo leo. Maisha yanajumuisha uchumi wa mtu, utamaduni, siasa, teknolojia na kadhalika.
Makala haya yanaangazia maisha ya Mtanzania tangu mwaka 2021 na kuendelea yakilenga uchumi wake. Maisha ya Mtanzania yamepanda kimatumizi kuliko kipato licha ya kutafuta kila mbinu za kujikwamua ili kupambana kiuchumi lakini imekuwa ni ngumu hasa mwananchi wa chini.
Uchumi huu utatazamwa katika maeneo makuu yafuatayo:
1. Tozo za Miamala kwenye Simu
Miamala ya simu ilikuwa ni mkombozi mkubwa wa watu wengi Tanzania hasa waishio vijijini kulingana na uchumi wao kuwa hafifu. Walitegemea na wanaendelea kutegemea miamala ya simu kama njia kuu ya kupokea fedha na kutuma fedha. Hongera kwa makampuni ya simu kwa kuwafikia watu wengi. Uchumi wa wengi ulianza kuimarika na kuwa na nguvu.
Mwaka jana 2021 July mambo yakaingia sumu kuvu ya tozo tena tozo kubwa, kwa mtumaji na mpokeaji. Serikali haikutazama ni kwa namna gani raia wake wataathirika waishio vijijini, vijana waliojiajiri baada ya kukosa ajira miaka 6. Biashara ya fedha kupitia miamala ya simu ikaanza kudorora huku gharama za maisha zikizidi kupaa. Haikutosha hapo, baadhi ya wananchi wakasema ni afadhali kusafirisha fedha kuliko tozo hizo. Wananchi wengine wakakimbilia kwenye benki. Mambo yakazidi kuharibika, huku gharama ya chakula, gharama ya mafuta ya kula, gharama ya mafuta ya vyombo vya moto haishikiki kila uchao. Serikali inaweza kudhani kuwa imesaidia jamii kwa kiasi fulani lakini maisha ya raia yamezidi kuwa mabaya kuliko vipindi vingine vilivyowahi kupita.
2. Tozo ya Majengo kupitia Luku
Tozo za majengo umekuwa mwiba mkubwa hasa kwa wapangaji. Kila mwezi elfu moja hukatwa kwenye umeme kaya ambazo hazijaingizwa kwenye mipango miji zimekuwa kwenye uonevu wa hali ya juu kwa sababu ya sheria kuwabana wenye umeme peke yake ilhali wasio na umeme hawawajibiki kwa sheria hiyo kwa sababu tu hawatumii umeme. Hivyo kuna majengo yanayolipa kodi ya jengo kwa mfumo wa luku, lakini kuna kaya ambazo hazilipi kodi ya majengo kwa sababu haziko kwenye mfumo wa luku au kutoingizwa kwenye mipango miji.
3. Tozo za Miamala ya Kibenki
Serikali mwaka huu imepitisha tozo kwenye miamala ya kibenki. Hili linazidi kuumuumiza mwananchi. Fedha zinazopelekwa benki zinakuwa zimekatwa kodi, tuanze na mfanyakazi amelipa kodi kulingana na kipato chake, serikali imechukua sehemu yake ndani ya mshahara huo. Benki kuna makato ya miamala kutokana kutoa fedha, za kitabu cha leja, serikali haijarizika na kodi iliyoikata, bali inapeleka tozo benki kwenye fedha iliyozikata kodi. Huu ni uporaji wa fedha za mwananchi, huu ni uonezi uliokithiri, serikali inatuonesha kuwa haina fikira pambanuvu za kukusanya mapato bali ni kuchukua kila alichonacho mwananchi.
Ukigeukia upande wa biashara, serikali inataka kodi na inapewa, lakini sasa mzunguko wa fedha uko wapi? Biashara zimedorora, kodi zinahitajika, tozo za benki kwenye viakiba vilivyo zinazidi kumpunguzia uhai huyu mwananchi.
Fedha inapatikana kwa shida kubwa huku matumizi yakiwa makubwa kuliko mapato. Sera na utekelezaji wake haviendani na maisha ya Mtanzania. Viongozi wa serikali tunaweza kudiriki kusema hamna uchungu na raia wenu kutokana na mwenendo wa tozo ambazo kila kukicha mnaziibua.
4. Mzunguko wa fedha
Katika mwaka 2021 hadi sasa mzunguko wa fedha umekuwa hafifu ukilinganisha na hali ya maisha ilivyopanda. Ni dhahiri kuwa serikali bado haina takwimu sahihi juu ya maisha ya mtanzania. Kuna baadhi ya mazingira ya kiuchumi kuipata elfu moja kwa siku ni ngumu huku bidhaa za kila siku zikipanda gharama mara dufu. Tunahitaji kujua sera ya mzunguko wa fedha mtaani ikoje na wanaitekeleza vipi? Serikali itueleze ni kwa nini madini na utalii havijawa vyanzo vikuu vya mapato na badala yake kodi na tozo kwa wananchi? Kwa nini nyakati zote hizi mwananchi amebebeshwa mzigo mzito namna hii kuliko uwezo wake? Lazima Bunge kama mhimili wenye kutetea maslahi ya wananchi watuhojie hili swali kwa serikali.
5. Nyongeza za mishahara kwa wafanyakazi
Serikali itambue kuwa nyongeza ya mshahara kwa mfanyakazi ikiwa ile itokanayo na sheria ya ongezeko la mshahara la kila mwaka, kupanda daraja au ongezeko litokanalo na mjadala wa bajeti ya mwaka, ni nguzo muhimu kwa raia wake. Mfanyakazi anategemewa na mfanyabiashara na mkulima. Ikiwa matumizi ni makubwa kuliko mapato hapo tunatarajia biashara za maendeleo kama ujenzi, urembo, mavazi basi biashara hudorora. Lakini inapofikia biashara ya vyakula nayo inadorora basi hali ya kiuchumi imekuwa ni mbaya zaidi. Kwa sababu binadamu ana jukumu la kila siku ambalo ni kula na kunywa, hayo mengine hufuata. Sasa huyu mfanyakazi asipofanyiwa vyema mfanyabiashara atashindwa kuwa daraja kiwandani na shambani kwenye kilimo kwani mzunguko wa fedha unategemea mwingiliano wa pande tatu zote tatu.
Fauka: kwa mapenzi ya dhati kabisa serikali tunaomba sana kuzingatia maisha halisi ya mtanzania. Maisha yake ni magumu kuliko vipindi ambavyo inadhaniwa. Wengi hawana pa kusemea wala pa kuanzia ila hali sio nzuri kiuchumi.

Upvote
3