taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 540
Najaribu kufikiria jinsi bei ya bidhaa zinavyopanda kwa kasi ikilinganishwa na kipato halisi cha Mtanzania. Wakati wa siku za mwisho wa juma nilizunguka kwenye maduka ya mtaani kupata mahitaji ya nyumbani lakini nilishtushwa mno kwa bei nilizozikuta; mfano:
1. sukari shilingi 2,000/kilo
2. mchele shilingi 1,600/kilo
3. maharage shilingi 1,900/kilo
4. nyama shilingi 5,000/kilo
5. mafuta ya kupikia sh. 4,000/lita
6. gesi ya kupikia sh. 47,000/mtungi
7. maji sh. 200/dumu
Nikiangalia hali hii na kauli za JK wakati wa kampeni za "ARI ZAIDI", "NGUVU ZAIDI" na "KASI ZAIDI" sipati picha ya mustakabali wetu Watanzania.
Tutaweza kweli kuyamudu maisha ikizingatiwa kwamba mahitaji mengine ya msingi kama matibabu, elimu kwa watoto, umeme na mengineyo bado yanatukabili? Waungwana naomba ushauri katika hili.