Maisha ya mwana JamiiForums nje na ndani ya JamiiForums

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,258
Reaction score
20,386
Asalaam wanajukwaa!!

Katika kutumia mtandao huu ( jamiiforums) mzuri na ninaoupa kipaumbele sana nimepata uzoefu na maswali mengi yakinizunguka akilini mwangu kuhusu members wa hii familia ya jamiiforum.
Kutokana na maswali hayo yalinipa hitimisho ama uzoefu mpya kabisa!!

Kiukweli namna watu wanavyojipambanua humu, ni tofauti kabisa na hali zao zilivyo, nafafanua kwa kila kundi ama jinsia kama ifuatavyo:-

1 KUNDI LA WANAUME WA JF.
Wanavyojisifu:-
I/wengi kama sio wote wana miliki magari au usafiri mzuri, yaani wengi hawapandi daladala kwenda kazini ama majumbani Kwao

ii/ wengi kama si wote wana kazi nzuri zenye mishahara mizuri, hapa utakuta watu wanabeza hasa wenzao wanaolipwa mfano laki Tatu au mbili kwa mwezi.
iii/ wengi kama sio wote ni watu wa vitengo ( usalama wa taifa na wanajeshi)[emoji23] [emoji23] [emoji23]
iv/ Hakuna asikari polisi hata mmoja humu jamiiforum, huwezi kukuta mtu akijipiga kifua humu kuwa yeye ni polisi ila tuna wajeda karibia wote humu[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87]

v/ Humu walimu wanadharaulika kwa sababu wanalipwa kidogo. Hivyo hatuna member ambao ni maticha humu labda tupate Leo.
vi/ wanaume wote wa jamiiforum hawatumii TV za chogo majumbani/ maghetoni Kwao, wao wana flat screen TVs ( smart TV) za bei kubwa hivyo yeyote anayetumia TV ya chogo huhesabiwa mlalahoi wa jf.

2.KUNDI LA WANAWAKE.
I/wote ni warembo, yaani vibinti vibichi.
ii/ wote wana K mnato.
iii/ wote ni wahitimu wa kuanzia shahada ( degree). Humu jf hakuna mwanamke mwenye elimu darasa la saba au form four.
iv/ kuwahonga mademu wa humu jamiiforum labda uanzie laki mbili na si chini ya hapo.
v/ wengi kama sio wote wamepanga nyumba nzima yaani apartment.
vi/ vinywaji vyao ni saint Anna, savanna, Grants, na castle lite kwa Mara chache.
vii/ Hakuna majimama humu jamiiforum, wote ni vimwana wazuuri.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]

HITIMISHO.
Kijana mwenzangu usijaribu kushindana na mazuri ya jamiiforum, kwani huu ni ulimwengu wa waliofanikiwa ( the world of granted).
Ingia shambani lima, fundisha, cheza italipa zaidi.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Sasa wee jamaa unachoshangaa ni kitu gani? Unataka tutumie ID fake lakini tuwe halisi? Mtaani kunabaki kuwa mtaani na JF yanaishia JF.

Hata hivyo iwe mtaani au JF, usijilinganishe na mtu mwingine. Usimchukie bila sababu anaekuzidi, chukulia kama changamoto ufanye vizuri zaidi yake.

Hali kadhalikabusimdharau unaemzidi, ongeza bidii usirudi huko.
 
Hata Insta Facebook SnapChat mambo ni haya haya. Unakuta mdada anapost kila siku yupo Cape town Fish Market ila hata pa kuishi hana anaishi kwa mashoga. Ukiishi kwa kutegemea maisha wanayoishi wengine kwenye social media unaweza ukawa shoga au punda au malaya. Turidhike na tulipo. Tupiganie maendeleo kwa faida yetu sio kwa sababu ya fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…