Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Uhiari wa chanjo ya COVID-19 uendelee kuheshimiwa. Maisha ya mwanachama wa chama cha siasa sio mali ya chama. Kwa CCM (au chama kingine chochote) kuweka msimamo wake kuhusu hii chanjo kusichukuliwe kumaanisha kwamba mwanachama mmoja mmoja wa CCM (au chama kingine) haruhusiwi kuwa na msimamo unaotofautiana na wa chama chake, hata kama hakisemei hicho chama.
Mimi sijamsika anti-vaccine crusader yeyote akikisemea chama chake. Juhudi zozote za kuwanyamazisha anti-vaccine crusaders ni juhudi za kukiuka dhana ya uhiari wa hii chanjo. Hata kama wanaipinga hii chanjo hadharani waachwe wafanye hivyo, kwasababu hata wanaoiunga mkono nao wanafanya hivyo hadharani.
Lectures zote zinazotolewa na crusaders wa kambi zote mbili zinaangukia kwenye “akili za kuambiwa”, ambazo Watanzania watachanganya na za kwao na kuamua, kila mtu kivyake vyake, whether achanje au asichanje. Kila crusader yuko sahihi kwa mujibu wa uelewa wake na imani yake. Hata kwenye eneo la dini tuko hivyo. Kila mwenye dini yake anamini kwamba dini yake ndiyo dini sahihi ya kumwabudu Mungu.
Hiari iachwe itamalaki.