MAISHA ya mwanadamu yana UKOMO

MAISHA ya mwanadamu yana UKOMO

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
SOMO LA LEO
MAISHA ya mwanadamu yana UKOMO.

"Tumezaliwa" "Tunaishi" "Tutakufa"

Huu ndio ukweli halisi wa maisha yetu.
Neno la Mungu katika kitabu cha AYUBU 14:1-2 linasema
" Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."

Kumbe maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Haijalishi tunaishi kwa siku ngapi, miezi mingapi au kwa miaka mingapi lakini hakuna atakayedumu milele. Kila mmoja ana siku yake ya mwisho.

Lakini hatakama tunafahamu hivyo lakini binadamu tumekuwa ni watu wa kujisahau mno. Tunasahau kwamba yupo Mungu muumbaji ambaye tunapaswa kumuabudu na badala yake tumekuwa bize sana kutafuta pesa au kufanya shughuri nyingine pasi na kumkumbuka muumbaji wetu hata kwa kushukuru kwa zawadi ya uhai na kile anatojuhalia kila siku katika maisha yetu.

Neno la Mungu katika kitabu cha MHUBIRI 12:1 linasema
"Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo."

Hapa neno la Mungu linatukumbusha kumkumbuka Mwenyezi Mungu wakati tungali tuna nguvu na uwezo wa kuomba, kusifu na kuabudu kabla haujafika ule wakati ambao hatutaweza kufanya chochote.

Haya maisha tunayo angaika nayo kila siku, hizi pesa tunazo sumbuka nazo kila siku hadi tunadhurumu nafsi za wengine mwisho utafika hatutaondoka na chochote. Kila kilichotuweka bize tutakiacha hapahapa duniani.

Simaanishi kwamba tuache kutafuta pesa, hapana. Tuendelee kuzitafuta na kumtolea Mungu sadaka na kusaidia wengine lakini kutafuta huko kusitufanye tuache kumcha Mwenyezi Mungu na kutenda maovu.

Neno la Mungu katika kitabu cha AYUBU 28:28 linasema
"Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu."

Hivyo, kila mwanadamu kwa kutambua kuwa maisha yake hapa duniani yana ukomo basi ni jukumu la kila mmoja wetu kujitenga na uovu na kujitengenezea azina iliyo njema kwa muumbaji wetu.

MAISHA ya mwanadamu yana UKOMO, tusijisahau kama kuna MUNGU aliyetuuumba, ambaye sisi sote tunapaswa KUMWABUDU yeye.

Hilo ndio somo langu kwa siku ya leo. Nikutakie tafakari njema.

AHSANTE.
______________________

It's me
A Lawyer and LifeCoach
[Mwanasheria na Mwalimu wa maisha]
Mr. George Francis
Phone: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Ni sahihi kabisa mwalm Bwana akubariki Sana...
 
Back
Top Bottom