Maisha ya Nikola Tesla na mawazo ya kusambaza umeme wa wireless bure dunia nzima

Maisha ya Nikola Tesla na mawazo ya kusambaza umeme wa wireless bure dunia nzima

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
MAISHA YA NIKOLA TESLA NA MAWAZO YA KUSAMBAZA UMEME WA WIRELESS BURE DUNIA NZIMA

Nikola Tesla alizaliwa julai 10 mwaka 1856 huko Smiljan Austria Empire ambayo kwa sasa ni Croatia akiwa ni mtoto wa nne kwa wataoto wa tano wakike watatu na wakiume wawili na Milutin Tesla (1819-1879) na mama Georgina Mandic (1822-1892) wote wakiwa na asili ya serbia, baba yake tesla alikuwa pastor katika kanisa la ki orthodox Croatia na mama alikuwa na kipaji cha kutengeneza vyombo vya nyumbani na vifaa ya mechanical pia akiwa amekariri mashairi baadhi ya kiserbia

Alipata elimu yake kwenye chuo kikuu cha Graz ambacho kwa muda huo kilijuwa kama (M.I.T) kwa Austria akisomea engineering na physics ingawa hakupata degree mwalimu wake aliwahi kusema kuwa Tesla alikuwa ni Genius kwenye upande wa hesabu

Aliwahi kufanya kaz chini ya Tivadar Puskas kwenye kampuni ya telegraph mwaka 1881 huko budapest kisha 1882 bwana Tivadar Puskas alimtafutia kazi Tesla huko Paris kwenye kampuni ya Continetal Edison iliyokuwa ikimilikiwa na Thomas Edison, Tesla alipata uzoefu mkubwa kwenye Electrical na Engieering na mameneja waliona juhudi zake na kumwambia awe ana design na kuunda dynamos na motor. Mwaka 1884 meneja Charles Batchelor alienda marekani kwende kusimamia kampuni ya Edison Machines iliyo chini ya Thomas Edison akiwa anaenda aliomba aende na Tesla kwenye kampuni hiyo hivyo mwaka huo Nikola Tesla akahamia rasmi marekani, alifanya kazi kwenye kampuni hiyo kwa miezi sita kisha akaacha ingawa haijawa wazi nini chazo halisi cha kuacha kazi hiyo ila inasemekana ni mshahara mdogo huku wengine wakihisi sababu ni kuwa kuna siku Tesla alisema alishawahi kuambiawa na Edison atengeneze vifaa ishirini na nne (24) tofauti tofauti vya standard machine kwa dola za marekani 50,000 ila baadae Edison akaja kumwambia kuwa huo ulikuwa ni utani tu.

Alianzisha kampuni yake ya Tesla Coil pia katika siku zake vitu alivyowahi kuvumbua moja wapo ni kutengeneza boti unayoweza ku control kwa wireless pia alitengeneza vifaa kadhaa vya mawasiliano visivyotumia waya (wireless) kama redio na simu

Mwaka 1901 alipata uwekezaji wa kiasi cha dola za kimarekani (150,000) ambazo kwa sasa ni sawa na (5,493,600) kwa uwiano wa sasa na J.P. Morgan ili atengeneze mnara wa mawasiliano wenye futi 90 alioupa jina la Wardenclyffe Tower huko colorado springs, J.P. Morgan alikuwa kaenda ulaya ila alipo rudi alikuta Tesla kaongeza urefu wa mnara kutoka futi 90 mpaka futi 180 na Tesla kaishiwa na hela hivyo Morgan alisitisha uwekezaji ila hakuishia hapo tu alihakikisha Tesla hapati pesa kwa wawekezaji wengine. Inasemekana kuwa tatizo la kujitoa ni kuwa alikuwa na hofu kuwa huenda mpango wa tesla wa kusambaza umeme wa bila nyaya ukawa kweli na yeye alikuwa na shamba na kampuni ya kutengeneza raba zinazotumika kwenye nyaya na mgodi wa copper hivyo angeharibu biashara yake sababu yeye anahitaji nguzo za mawasiliano na nyaya za mawasiliano afanikiwe kwenye biashara yake. Kama Tesla angefanikiwa kutengeneza mnara huo alikuwa na mpango wa kusambaza umeme kwa kutumia wireless bure mwaka 1917 baada kusitishwa kwa ufadhili mnara ulivunjwa.

Baadhi ya watu wanasema Tesla aliamini pyramid kuu zilizopo misri ( THE GREAT PYRAMID) hazikuwa sehemu ya kuweka miili ya viongozi wa misri bali ni majengo ya kusambaza umeme wa wireless kwa wananchi wao hivyo alijenga mnara wa Wardenclyffe kwa kuangalia misini ya pyramid.

Tesla aliwahi kusema kuwa Atoms zinafanyakazi kama solar system na pia mwanga unaweza kuwa kama Particles au Waves hakupewa tuzo ila Einstein alipewa Nobel prize kwa kusema mwanga unafanya kazi kama particles pia mwanasayansi Rutherfold alipata Nobel prize kwa kusema Atoms zipo kama solar system ndongo, Tesla katolewa kwenye historia ya wana Quantum physics.

Mwaka 1937 akiwa na miaka 81 Tesla mida ya usiku alitoka nje ya hoteli yake kwenda maktaba akiwa anavuka barabara aligongwa na gari aliyomtupa chini na aliumia mgongoni na alivunjika kama mbavu tatu ingawa majeraha halisi hayakuwekwa wazi na Tesla alikaa kwenda hospitali hivyo hakupona kabisa. January 7 1943 akiwa na miaka 86 Nikola tesla alikutwa akiwa amekufa na mfanyakazi wake kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa anaishi.

Jeshi la marekani lilingia chumbani kwake na kuchukua kila kitu cha Tesla ikiwemo document zake na walikaa nazo kwa muda wa miaka kumi toka 1943 mpaka 1952 ndipo walipo viachia vitu vyake na inasemekana kuna baadhi ya document zilipotea na hajizapatikana mpaka sasa hivi

Kwa sasa huku Belgrade Serbia kuna museum ambayo inahistoria na taatifa ya maisha na taarifa za uvumbuzi wa Nikola Tesla
 
Kuna ile silaha moja alitaka kuunda, kama sijasahau ni beam death au death ray kama itakuwa sijakosea, silaha inayoweza kuangusha ndege nk kirahisi kabisa na hata kama Kuna invasion kutoka space basi inaweza tumika, nadhani US washaidevelop na kufika mbali na inawezekana ni miongoni mwa secret weapon walizonazo US...marekani si mpumbavu kuweka mazingira ya kuvutia talents mbalimbali nchini kwao, faida halisi ya hizo talents hufaidisha zaidi marekani zaidi ya tunavyofikiri.
 
Kuna ile silaha moja alitaka kuunda, kama sijasahau ni beam death au death ray kama itakuwa sijakosea, silaha inayoweza kuangusha ndege nk kirahisi kabisa na hata kama Kuna invasion kutoka space basi inaweza tumika, nadhani US washaidevelop na kufika mbali na inawezekana ni miongoni mwa secret weapon walizonazo US...marekani si mpumbavu kuweka mazingira ya kuvutia talents mbalimbali nchini kwao, faida halisi ya hizo talents hufaidisha zaidi marekani zaidi ya tunavyofikiri.
Hiyo nilisikia pia ni death ray nahisi kuna msemo alishausema mwenyewe kuwa "yesterday is there's and today is mine"
 
Back
Top Bottom