---maisha ya "njozi za kutisha"--

halafu tulizo.................
 

...ashadii upo ndani ya msitari kabisa, la general....kitendawili chenyewe hakina hata jibu hata umalize miji yote ya bara na pwani...tulizo...haya ngoja nikujibu jibu ambalo litawajibu nyote nilio wa quote....

hivi baada ya mgao wangu wa mwisho wa mwezi kuugawa kwenye wizara zifuatazo;
1. chakula na lishe, 2. usafiri, 3. nishati mkaa, mishumaa, mafuta ya taa na luku, 4. elimu ada, vitabu, etc 5. mawasiliano vocha, etc
hapo hujavaa, hujachangia kitchen party wala harusi, ....mbaya kuliko zote, wizara ya afya na dharura
ulichowekeza ni panadol tu na dawa mseto ya malaria...
--- halafu unalaumiwa eti mbona humalizi ujenzi---....hii ni halali kweli?

watu hao hao wanakwambia 'mwezi huu unatakiwa unisaidie mimi mzee wako milioni moja nikarabati duka langu, ndio kiinua mgongo changu na mama'ko!"...yaani unajua hiyo milioni hata ukiwekeza huna hisa, wala si mkopo tuseme utapata riba!
aisee...acha tu...kuna watu wakihadithia maisha yao utachoka!

na hii haijalishi anapokea 75,000/= , ...au milioni/=
the more you earn the bigger the demand!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…