Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama

Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITABU KIPYA: UISLAM ULIVYOINGIA UCHAGGANI

Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtoto mdogo wakati Wamishionari wanaingia Kilimanjaro baada ya Mkutano wa Berlin mwaka wa 1884 na Wajerumani wakaingia Uchaggani kuanza kutangaza Injili wakati huo jina alilopewa na baba yake lilikuwa Kirama Mboyo.

Baba yake aliyejulikana kwa jina la Muro Mboyo alikuwa Jemadari wa Majeshi ya Mangi Ndeseruo Mamkinga wa Machame.

Sintofahamu baina ya Mangi na Jemadari wake ulisababisha Jemadari Muro Mboyo kwenda kuishi uhamishoni Old Moshi kwa Mangi Rindi Mandara na mkewe aliyekuwa anaitwa Makshani Olotu kurudi kwa wazazi wake Kibosho kwa Mangi Sina akiwa na mwanae mdogo Kirama.

Huyu mtoto mdogo Kirama alipokuwa mtu mzima na akauingiza Uislam Uislam Machame mama yake Makshani aliupokea Uislam na jina lake likawa Sauda na baba yake aliporudi Machame wakati wa utawala wa Waingereza na yeye pia alitoa shahada na jina alilochagua ni Ibrahim, ''Rafiki wa Allah.''

Kuna mengi aliyopitia Rajabu Ibrahim Kirama katika harakati zake za kuupigania Uislam akipambana na Mangi wa Machame wa wakati ule Abdiel Shangali akizuiwa kujenga msikiti na alipojenga ukavunjwa kwa amri ya Mangi.

Alipambana na Waingereza wakati anataka kujenga Muslim School ya kwanza Uchaggani akinyimwa misaada ya fedha ambayo serikali ilikuwa inatoa kwa Shule za Misheni.

Kwa ustadi mkubwa Rajabu Ibrahim Kirama alisafari hadi Zanzibar kutoka msaada kwa Sayyid Khalifa bin Humud na kukutana na Sheikh Hassan bin Ameir na kuweza kuunga udugu na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ya Dar es Salaam na kufungua tawi Machame Nkuu kijijini kwake.

Historia hii haikamiliki bila kutaja ukoo wa Marua na haikamiliki kamwe bila kuwataja vijana wadogo wanne waliotoka Zanzibar kuja Uchaggani na Upare kusomesha Qur'an - Shariff Allawi, Sheikh Mahmud Mshinda, Sheikh Abdallah Minhaj na Sheikh Saleh Mwamba.

Historia hii imechelewa kuandikwa na ndani ya kitabu hiki mna mafunzo mengi lau yaliyotokea inafika sasa zaidi ya miaka 300 historia hii ikihadithiwa kutoka kizazi hadi kizazi.

RAJAB IBRAHIM KIRAMA (1833 - 1961).jpeg
 
Safi Sana Sheikh Mohamed kwa majitoleo yako ya kutafiti na kuandika historian mbalimbali
 
Back
Top Bottom