Maisha ya simba dume yamejaa misukosuko hakuitwa mfalme wa nyika kwa bahati mbaya

Sehemu pekee simba dume anapohusishwa kwenye kuwinda ni pale simba wanapowinda nyati mkubwa. Simba dume kutokana na nguvu zake ndio anayemkaba pumzi mpaka afe pale simba jike wanapokuwa tayari wamemshikia chini.
 
Sehemu pekee simba dume anapohusishwa kwenye kuwinda ni pale simba wanapowinda nyati mkubwa. Simba dume kutokana na nguvu zake ndio anayemkaba pumzi mpaka afe pale simba jike wanapokuwa tayari wamemshikia chini.
Kweli pindi wanapowinda mnyama mkubwa kama twiga hata tembo mara nyingine simba dume lazima ahusike sababu ya nguvu na uzito wake hurahisisha kukalisha wanyama hao ,nyati pia hivyo hivyo jike 5 wenyewe kwa nyati aliyeshiba wanatoka jasho kumuangusha


Swadakta
 
kumbe hata simba hataki kuishi na watoto wasio wake kama ilivyo kwa binadamu
 
Nimependa jinsi ulivyomuelezea simba dume!!
 
kumbe hata simba hataki kuishi na watoto wasio wake kama ilivyo kwa binadamu
Tena hataki haswa bora ya binaadamu


Akishatwaa eneo na akakuta jike ana vitoto basi anawaua watoto wote ,kisha wataanza maisha mapya na kuzaa watoto wenye damu yake ndio maana jike hutafuta dume lenye nguvu kwaajili ya kumlea yeye na kuwalinda watoto
 
Hiyo misukosuko si ya mchezomchezo
 
Umesema ukweli mtupu juu ya tabia na maisha magumu yanayowakabili simba dume. Hata hivyo, eneo lao la kiutawala nadhani huwa lina umbali mrefu wa hadi maili 10 kwani akiwa na eneo dogo hawezi kupata chakula cha kutosha maana unajua jinsi wanyama wala majani wanavyohamahama na kujikuta wakitegemea zaidi mbogo (Nyati) ambao wao wanapatikana tu karibu na vyanzo vya maji. So kwa kuwa kwenye mbuga maji huwa yako mbali mbali, hivyo Pride inalazimika kuwa na eneo kubwa la sivyo watakuwa wanapigana na kambi nyingine kila siku kwa kutrespass.
 
.....

Simba hawindi swala ni aghalabu sana simba kuwinda swala sababu swala ana mbio sana na simba hana mbio za .....

...

Simba huyu asipopata jike maana ni aghalabu sana kumuona simba jike awe pekee yake basi atatakiwa aingie...

Aghalabu maana yake ni mara nyingi.

Nadra maana yake mara chache.

Tusiharibu kiswahili.
 

Kuna Blue Ray Disc inaitwa :Animals Battle Field". Ukiipata hii unakuwa umemaliza kila kitukuhusu wanyama, mpka Polar Beers. Ni utafiti uliofanywa na NATIONAL GEOGRAPHIC CHANNEL kwa njia ya Satellite kwa takribani miaka 50. Hii Disc ina picha ambazo ukiamua kuziandalia mfululizo bila kupumzika, inaweza ikakuchukua si chini ya miezi mitatu kuzimaliza. In fact it has everything. Mimi nilibahatika kuinunua kwa Machinga miaka ya nyuma kwa bei ya Tshs 2000/= tu . Ni nzuri hakuna mfanao!
 
Aise! inaonekana ni tamu sana hii,Kwa sasa itapatikana kweli mkuu,Mimi huwa napenda sana kuangalia hizi mambo,Hasa weekend.
 
Aise! inaonekana ni tamu sana hii,Kwa sasa itapatikana kweli mkuu,Mimi huwa napenda sana kuangalia hizi mambo,Hasa weekend.
Unaweza ukacheki na hawa machinga wanaouza DVD za kubeba mikononi. Ebu ngoja nione kana naweza kupata kipande chake halafu nitakuwekea hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…