SoC04 Maisha ya Tanzania baada ya mwisho wa dunia: Post apocalyptic Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Ni siku kama siku nyingine bodaboda zimejazana mtaani, jua limewaka, upepo unapuliza kwa kasi inayotimua mchanga na vumbi kiasi. Kiangazi kichanga kabisa. Kwa mbali wanaonekana watu kadhaa wakitembea uchi wa mnyama! Hawana wasiwasi wa kuonwa na waliovaa nguo maana wanatambua kuwa kila mmoja anaelewa maana ya wao kufanya hivyo. Wapo uwazi wanachokiwaza na wanatenda wanachoamini bila kuomba radhi mara miamia.

Katika jamii hii kila mmoja anajieleza anachowaza na anaeleweka. Hapana ulazima wa kufuata wazo asiloliafiki mtu binafsi, tunaelewana na kuchukuliana na kuvaa viatu vya wengine. Hivyo walio uchi wameamini kuwa wazi na kuirudia hali ya Edeni ndio asili iliyo njema na wameifuata. Sisi wengine tumeamua kubakia na uvaaji wa nguo. Wote ni sawa, wote tunaishi pamoja katika jamii inayoaminiana, kuheshimiana na kuchukuliana kibinaadamu kikamilifu. Mjadala baina ya kuvaa au kutovaa nguo ni endelevu, kila upande umejizatiti kwa pointi. Wapo wasiochagua upande wanaoamua kutoka na fasheni (uchi vs nguo) iwapendezayo siku hiyo. Usishangae sana, japo inashangaza! Hayo ni mojawapo ya masuala ya kawaida kabisa hapa baada ya mwisho wa dunia Tanzania na Africa kiujumla.

Sifa nyingine za jamii hii ni;

1. Imani ya kwamba hali iliyopo ndiyo hali njema na mazingira murua kabisa.
Imani ya kwamba watu tuliofanikiwa kuzungukwa nao ndio haswaa tunaowahitaji, hakuna anayewaonea uchungu waliokufa maana kila mmoja anaonekana kuamini kwamba wafu wasingepapenda hapa katika jamii yenye uwazi, uwajibikaji, upendo na ujamaa wa namna hii.

2. Wote tunaishi bila wasiwasi wa kuzeeka na kufa, tunaamini kuwa uzee na kifo ni vitu sahihi tena muhimu kwa wakati wake. Kimsingi mtoto anaupenda utoto wake anaouishi kikamilifu, mzee pia anaupenda uzee wake na kuuishi KIKAMILIFU.

Kila mmoja amehuishwa tena katika umri ule anaoupenda zaidi. Binafsi nipo katika hali ya umri niliokuwa nao pindi nilipomaliza shule ya upili ya advansi, miaka 21. Kijana mwenye mafikirio makubwa, mwanasayansi wa haswahaswa! Ndiyo maana nimepanga, nitaiishi jamii hii nikiwa kama muandishi wa kitabu cha muhubiri. Kujaribu kuwatanabaishia watu kipi ni kipi? na kipi haswaa chafaa;

1. Kila mmoja aelewe kwamba katika jamii hii la maana ni kuwa mshiriki muhimu kama mwanajamii. Kutimiza nafasi yako ya kuwatumikia watu. Kila mmoja anatamani kutumia alichonacho kujinufaisha kwa kuwatumikia wanajamii wenzake. Ndiyo maana mzee anatamani na kupenda sana kuombwa ushauri wa busara zake. Anaendesha maisha kwa kazi hiyo ya Mshauri. Kijana anatumia nguvu zake kujenga jamii bora kiubunifu, michezo na burudani. Nao watu humlipa vizuri kila mmoja akafurahia.

2. Hakuna mtu anayetamani kuibia ama kumnyonya mwenzie. Fikiria mfano: zipo nyumba ambazo zimebakia bila watu sababu hayupo hata mtu mmoja aliyeponea chupuchupu kuokoka kutoka familia hiyo. Lakini hakuna mtu anazishobokea kuzirithi. Watu hudhani labda atakuja kutokea mrithi halali kutokea mbali aje azirithi.

Hiyo ni kinyume kabisa na mafikirio ya zamani, ilihisiwa kutatokea uwizi na uvunjifu mkubwa wa amani.
Hili limetokana na ukweli kwamba, badala ya wenye mapenzi mema kuondolewa duniani kwa kunyakuliwa na kuwaacha wabaya watawale duniani (Hell-on-earth). Bali kilichotokea ni watu wabaya wamepotea na kuwaacha wema duniani (Heaven-on-earth)

2. Tambua katika mazungumzo na majadiliano, lengo la msingi ni kuuelewa ufikiri na wazo la huyo anayezungumza. Hivyo anapozungumza mmoja, mmoja anasikiliza ili aelewe sawasawa pande zote. Anavaa viatu vya mwenzie. Jamii hii imejaa watu waelewa mno. Wadadisi.

Vutia picha udadisi, maongezi na uelewa umefikia kiwango tunawasiliana hadi na wanyama wanaongea na kueleweka dhahiri kabisa. Si ajabu kukatiza mtaani na kumsikia mama-bata anawaambia wanae "Tangulieni mbele wanangu". Mbwa wanaagana "Tutaonana baadaye broh"!

Namna mwisho huu ulivyotokea:
Katika tukio la mwisho wa dunia, sio moto bali maji ndiyo yaliyohusika. Maji yale hayakuangamiza ki-gharika wala mafuriko maana yangeathiri uhai wote. Yale yalikuwa ni maji maalumu yanayoyeyusha na kuupoteza ubaya wa aina zote. Hivyo ilikuwa zaidi ni kama kuogelea katika ubatizo kamili. Mtu anapoingia anaoshwa na dhambi/ubaya yaani uchafu unabakia majini. Anatoka mtu saaafi asiyekuwa na marangirangi yaani transparent! Baada ya hapo anachukua umbile la umri na ubora aupendao na kuumudu kikamilifu anakuwa raia wa jamii mpya safi. Inasikika kama kubadili kabisa uwanda 'dimension', japo kiukweli ni dunia hiihii tuliyonayo. Anaamkia ulimwengu mwingine wenye watu wote wakweli, wanaoaminiana/ka na wanaotakiana mema kama majirani.

Jinsi waliojifungamanisha na dhambi wanavyopotelea majini: Fikiria mfano mzinzi katika maji yasafishayo:
maungo yake yatasomeka kama uchafu/dhambi hivyo yatayeyuka. Atajikuta akiishi atakuwa mlemavu mbinguni jambo ambalo haliwezekani hivyo mtu huyo atapotea mzimamzima. Mfano: kuwepo kaseti inayoharibu kila sehemu ya wimbo isiyokuwa injili (habari njema) ambayo wimbo kama Furaha ni kulewa na marafiki - Iyanii, unapita karibia wote, halafu wimbo wa Raha jipe mwenyewe wa Neema unaharibiwa hadi hautamaniki. Msingi ni ukweli wa mambo, maadili na mshikamano wa kijamii ndio unaozingatiwa.

Muasi-jamii anaweza kutubu, sehemu mbaya zikasafishwa akabadili akili akawa mwanajamii safi wa mbingu ya duniani. Mchakato wa kutubu utampatia maumivu makali sambamba na jinsi alivyojiungamanisha na tabia husika. Kama ambavyo mtu huumia kuipoteza sehemu ya mwili wake. Ni maumivu. Sasa fikiria muuaji muendelezaji: muuaji anatumia moyo, damu, mikono, miguu na akili kubwa kupanga na kutekeleza mauaji hivyo wakati wa usafishaji atajikuta mwili mzima umeyeyukia majini.

Moto mkali ungeweza kutumika kusafisha, maji yamependelewa kwa sababu ya upole wake ukilinganisha na ukali wa moto. Na ndugu zangu sio lazima maji au moto kutumika kuisafisha dunia. Uwezekano upo wa ugonjwa kutumika kusafisha jamii za ainabinadamu. Mfano: UKIMWI na kisonono vikasafisha uzinzi. Ebola ikasafisha ulafi. Ugonjwa unaofanania kisukari ukasafisha ubinafsi na mfanano wa presha ukawasafisha wasioaminiana na wanadamu wenzao. Upo uwezekano wa kutokea gonjwa moja jumuifu likatumika kama mbadala wa moto na maji kuitakasa dunia. Wewe pendelea tu mema, utaokoka.

Watu waliookoka muosho wa dunia walioko mabara yaliyoendelea wanatamani kuja kuishi nchi zinazoendelea kwa sababu huku watapata nafasi ya kujitanua zaidi, kuonesha uwezo wao katika kuzijenga jamii wanazoishi. Yaani aliyeokoka na kujikuta katika barabara ya lami anatamaaaani sana akaishi na jamii yenye barabara za vumbi ili aongoze matumizi ya rasilimali kujenga lami aache jina zuri machoni pa wanadamu na Mungu/Ulimwengu.

Endelea kuishangaa Tanzania (na Afrika) ya baada ya apokalipsi: Ndiyo itakuwa na bodaboda, barabara za vumbi tena zenye makorongo. Lakini pia ndio itakuwa nchi yenye raia wanaoishi kwa furaha isiyo na kifani! wakiiendelea kuijenga nchi yao pamoja. Tanzania tuitakayo.
 
Upvote 8
Ngoja tuone...

Cc: Mahondaw
Hahahahaaaaaah! Bwana Smart umenena vema.

Sema nn: on further examination, the kauli 'Ngoja tuone' inasaundi kama bado haijatokea itakuja baadaye. Wrong.

Huu mchakato unaendelea kila siku, kila siku mazingira na sie tunaujenga mwisho - na mwanzo mpya pia🤫
 
Duuh! Hii Tanzania tuitakayo ina mambo
 
Back
Top Bottom