Maisha ya uhalifu + utundu wa kutoroka gerezani ya mwamb John Herbert Dillinger

Maisha ya uhalifu + utundu wa kutoroka gerezani ya mwamb John Herbert Dillinger

Adil_101

Senior Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
110
Reaction score
345
PART 1:

[emoji100]Sio tu Marekani yote, we ukipata muda nenda kawaulize hata FBI kuwa huyu John Herbert Dillinger aliwafanya nini!!?, wasipokujibu nenda Kapitie Mafaili yao, Utapata majibu huko.
.
Dillinger alikuwa ni kiongozi wa kundi fulani la kihalifu lililofahamika kama, ‘Dillinger Gang’.
.
Kundi hilo linatajwa kuhusika na matukio mbalimbali, ikiwemo wizi katika benki zaidi ya 24 na pia uvamizi wa vituo vya polisi takribani 04.
.
John Dillinger alizaliwa June 22, 1903, pale 2053 Cooper Street, Indianapolis, Indiana.
.
Akiwa ni mtoto wa pili wa Mr John Wilson Dillinger (1864–1943) na Bibie Mary Ellen "Mollie" Lancaster (1870–1907).
.
Tabia chafu chafu za Dillinger zilianza kuchipua akiwa ‘Teenager’, ambapo mara kadhaa baba yake alisogezewa kesi za mwanae kupiga watoto wenzie na kuwafanyia ‘bullying’.
.
Dillinger aliacha shule mapema sana, na kisha akaanza kufanya kazi pale ‘Indianapolis machine shop’.
.
Baba yake na Dillinger akahisi kama kasi ya mitaa kumlea mwanae inazidi kuongezeka, hivyo akaamua kuihamishia familia yake yote kule Mooresville, Indiana mwaka 1921.
.
Huko sasa ndio mambo yakazidi kuwa mabaya, kwa maana mwaka 1922, Dillinger alikamatwa na Polisi kwa kosa la wizi wa vipuli vya magari, na hapo ndipo ukaribu wa yeye na baba yake ukayumba.
.
Kutokana na utundu wake wa kwenye vipuli vya mashine, Despite uhuni wake Dillinger aliajiriwa na United States Navy mwaka 1923 kama ‘Petty officer third class Machinery Repairman’.
.
Huko hakudumu sana, yakamshinda na akaona arejee Mooresville, ambako huko alikutana na bibie Beryl Ethel Hovious na kisha wakafunga pingu za maisha siku ya 12/04/1924.
.
Inasemeka mwana alijitahidi sana kutulia kwenye ndoa, ila inaaminika mambo ya ndoa yakawa kama yanamkataa hivi.
.
Kwasababu alikuwa ni Jobless, akaamua kumtafuta rafiki yake wa muda mrefu Ed Singleton na kisha wakapanga tukio lao la kwanza la uhalifu, na wawili hao wakafanikiwa kuvamia Grocery fulani, na kuiba kama $50 hivi.
.
Shuhuda Mmoja aliamua kutoa taarifa ya tukio hilo kwa Polisi.
.
Wawili hao wakakamatwa na polisi siku iliyofuata, Ed akasema yeye hakuhusika akakataa kata-kata, na kwa bahati mbaya/nzuri hakukuwa na vithibiti vyovyote eneo la tukio vilivyoweza kuthitisha kuwa Ed alihusika.
.
Ila kwa Dillinger, hali ilikuwa ni tofauti kidogo.
.
Siku ya tukio, Dillinger alimshambulia mmoja ya wafanyakazi wa kile ki Grocery kwa bolt ya mashine, kwaio kulikutwa na uthibitisho wa uwepo wake kwenye eneo la tukio.
.
Kabla hukumu haijatoka, Baba yake na Dillinger ambaye alikuwa ni mtumishi katika kanisa la ‘Mooresville Church’ aliongea na aliyekuwa mpelelezi wa kesi hio Omar O'Harrow, na wawili hao wakashauriana kumsihi Dillinger kukiri makosa ya kuhusika na tukio hilo, wakidhani labda hio ingesaidia kupunguza adhabu ya Dillinger baada ya hukumu.
.
Badala yake, kutoka miaka 10, Dillinger akachapwa miaka 20 Jela.
.
Baba yake alijitahidi sana Kumuomba hakimu ampunguzie adhabu mwanae, ila jitihada hizo ziligonga mwamba.
.
Mwana akatupwa Indiana State Prison Mwaka huo wa 1924
.
Mara tu ya kutupwa humo, katika siku za mwanzo kabisa, Dillinger aliwaambia wafugwa wenzake kuwa “I will be the meanest bastard you ever saw when I get out of here”.
.
Vipimo vya awali vya afya yake kama mfungwa, vilionesha kuwa Dillinger alikuwa na kipindupindu kikali sana ambacho hata matibabu yake pia yalikuwa ni special na yenye maumivu Makali.
.
Akiwa humo humo gerezani, Dillinger anakutana na wahuni wengine kama Harry "Pete" Pierpont, Charles Makley, Russell Clark, na Homer Van Meter, ambao wote hao kwa pamoja wanapanga tukio jingine la uhalifu wa kuivamia benki fulani, endapo kama watafanikiwa kutoka gerezani humo.

********** END OF PART 1 **********
Screenshot_20230420-202325.jpg
IMG_20230420_202902.jpg
IMG_20230420_203017.jpg
 
PART 2:
.
Kuna mwana alikuwa anaitwa Herman Karl Lamm, huyu alikuwa ni Mbobevu wa masuala ya kufanya wizi kwenye Mabenki na alikuwa na madesa yake kabisa aliyokuwa ameyaandika juu ya matukio hayo.
.
Huyu Herman Karl Lamm yeye aliishi kwenye miaka ya 1980 huko, na alifariki 16/12/1930
.
Kwaio kipindi yupo gerezani, Dillinger alikuwa akipitia madesa ya Herman Karl Lamm pia.
.
Baba yake na Dillinger akaanzisha movement ya kutaka kumtoa mwane gerezani, na petition yake ikapata sahihi kama 188 hivi, hivyo basi Dillinger akaachiwa huru May 10, ya 1933.
.
Kwa bahati mbaya sana, Dillinger aliachiwa katika kile kipindi cha
‘Great Economic Depression’, ambapo mifumo mingi ya kiuchumi ilikuwa imezorota.
.
Hivyo hakuwa na namna nyingine, ilibidi tu mwana arejee kwenye matukio ya uhalifu kama ilivyo kawaida yake.
.
June 21, ya 1933,Dillinger akafanikisha kuiba benki kwa mara ya kwanza na akajinyakulia kama $10,000 kutoka pale New Carlisle National Bank, tena akiwa peke yake.
.
August 14, akavamia na kuiba bank moja iliyopo pale Bluffton, Ohio.
.
Akakamatwa mara hii Allen County Jail ikamhusu
.
Wakati wanamkamata ili wakamtie jela, polisi walim-search jamaa na kumkuta na document ambayo ilikuwa na kichwa ‘Prison Escape Plan’.
.
Polisi walimsihi sana aseme lolote kuhusu hilo, ila jamaa akakataa kata-kata[emoji88][emoji3544][emoji419]
.
Kumbe baada ya kutoka kwenye lile gereza la kwanza, Dillinger alihusika kuchora mchoro wa kuwatoa na wale masela wake wote waliokuwa kule Indiana gerezani na alifanikiwa.
.
Na hao wote kwa pamoja ndio waliunda ile ‘The Dillinger Gang’.
.
Baada ya kuwasaidia wanae kutoka kule Indiana, walikuja kulipa fadhira na kisha wakamtorosha Dillinger kutoka kwenye gereza hilo alilokuwepo sasa.
.
Kundi hilo lilihusika kwenye matukio mengi sana ya uhalifu ikiwemo wizi wa mabenki na mauaji ya polisi.
.
Mwaka 1934, aliyekuwa FBI Director wa wakati ule, J. Edgar Hoover alimtaja John Dillinger kama “America’s very first Public Enemy No. 1.”
.
Dillinger alifariki 22/07/1934 Kule Chicago, Illinois.
.
Muwe na Eid Njema[emoji846][emoji736]
IMG_20230422_121048.jpg
IMG_20230422_121124.jpg
IMG_20230422_121208.jpg
IMG_20230422_121229.jpg
IMG_20230422_121303.jpg
 
Back
Top Bottom