Maisha ya usanii yanachochea kifo hapa Tanzania.

Maisha ya usanii yanachochea kifo hapa Tanzania.

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,033
1.Nimekua nikifanya utafiti kwa mda mrefu sana hatimae kuna kitu nimekihisi kwa wasanii wetu hasa upande wa muziki. Wengi wakishakua ma super star wanakua na maringo sana au hata kama hawana maringo baadae wakifulia/wakichuja inakua ngumu sana kwa wao kujichanganya na badala yake wanageukia madawa ya kulevya na ulevi walau kupunguza stress.

Wengi wa wanaotumia haya madawa sio kama wanapenda bali effect yao kwa mashabiki inawaumiza kichwa. Wengi hawadhubutu kujichanganya na jamii na kufanya kazi ili kujipatia kipato, wengi huwa wanatengeneza maisha yao yategemee mziki tuu sasa mziki usipouza ndio basi tena. Halafu wengi wao hawasaidiani, kwa mashabiki huwa wanasalimiana na kukumbatiana sana ila mambo ya ndani kama kusaidiana pesa hamna.

Kinachowamaliza ni kutojiamini hivyo hawadhubutu kujichanganya na jamii kutafuta pesa.

2.Unyonyaji.
Tumeona baadhi ya vituo vikubwa hapa nchini vinavyowawahisha kaburini wasanii wetu kwa kuwanyonya haki zao na kuwawekea masharti magumu. Kma ambavyo ishasemwa na wasanii wengi, Watanzania wengi wanafahamu hilo swala. Ile radio ya mawinguni iliyopondwa na Master J. na mimi ndiyo hiyo hiyo. Ni mafisadi sana hata sitaki kuwaona.
Najua Marehemu Ngwea alijihusisha na yale maswala baada ya maisha kumuwia magumu ila alipoingia huko mawinguni ndio akaharakisha kifo chake.
Navyoona mimi jamaa kama alijiua kuepukana na shida za ulimwengu. Ataenda wapi sasa wakati ni star, Ajichanganye na watu apige tofali na kuuza mgahawa apate pesa? No hilo najua hakuna mwenye ujasiri nalo na ndio maana wengi wanajimaliza.
Kwa wanawake wengi wamejiuza au kupiga picha za uchi ili wapate soko na kujiuza mwisho wa siku ukimwi unawamaliza halafu zinakuja sababu kibao eti moyo mkubwa, sijui presha kumbe wapi gono tuu limefichwa.

MWISHO.
Wasanii muache kuwekeza maisha yenu yote kwenye muziki bali mjijengee fursa nyingi kama kufungua biashara na kujiendeleza kielimu ili mlango mmoja ukifunga muhamie mwingine kama wanavyofanya wenzenu Mwana FA, AY, Profesa J, Sugu, Jafarai n.kn sio munakazia tuu muziki kana kwamba ndio kila kitu.

Wasanii muwe na upendo, msaidiane katika kila hali. musiwe wachoyo kama huyu ndugu yetu anaetamba sasa ivi asiependa kufanya kolabo na watanzania wenzie badala yake anachagua tuu anaowapenda.

Mashabiki tuwasapoti wasanii wetu kwa kununua kazi zao na kwenda shoo zao! hata kama huendi we mlipie hata rafki yako au lipa tuu pesa itamfikia.

Waimbaji muunde chama chenu na mkijenge kwa mfuko humo muwe mnasaidiana, wenzenu bongo muvi walishaunda kitambo ila sijajua utendaji wake kwa kweli.
Hayo tuu NAWASILISHA.
 
Pia muziki una haribiwa na Cloudz media, wana wanyonya wasanii sana.

*maisha wanayoishi wasanii wa bongo yalipswa kuwa bora sana kama sio uenevu na ubepari wanao fanyiwa
 
Pia muziki una haribiwa na Cloudz media, wana wanyonya wasanii sana.

*maisha wanayoishi wasanii wa bongo yalipswa kuwa bora sana kama sio uenevu na ubepari wanao fanyiwa
Kabisa, yani ningelikua msanii halafu nidhulumiwe haki yangu ningewaripoti mahakamani mara moja. Mifisadi naichukia sana, wapendwa kibao wametangulia mbele ya haki kwa sababu yao.
 
Back
Top Bottom