Naandika post hii nikiwa sijui pa kuanza, il a kwa kifupi tu, nimeanza maisha mapya ya kuwa single mother.
mimi na baba mtoto havijawork out kwa kweli na imenibidi nifanye maamuzi magumu. ni mwanaume nimekuwa nae kwa muda wa miaka saba ila hatujaoana, tumefanya mambo mengi ya maendeleao pamoja,ila gafla tabia yake ikabadilika akawa ni mtu wa kunigombeza bila sababu, chochote nikifanyacho kwakwe ni kibaya,lugha anayotumia kwangu akiwa na hasira ni mbovu, ila at the same time anasema ananipenda,nimekuwa ni mtu wa kuumia moyo kwa muda wote huo,najiuliza ni kupenda gani kwa namna hiyo.
Hivi karibuni nimeamua isiwe tabu kila mtu aendelee na ustaarabu wake,yeye amekuwa akitumia mtoto kunisema nina roho mbaya, sina huruma na maneno kedekede,ila kusema ukweli nimevumilia vya kutosha na sasa nimeona basi inatosha, ninampenda ndio na ingetokea miujiza abadilike ningemrudia ila ndo hivyo.kwa hasira amegoma hata kumuhudumia mtoto anasema akifika miaka saba nimpe sasa hivi akimuona atasikia uchungu kisa mimi simtaki.
Kwa wenye uzoefu jamani naanzaje kuishi maisha ya usingle mother wakati kila siku lazima mtoto aulizie daddy au hata akilia atalia daddyyy dadyyy,nitakuja kumwambia nini akiwa mkubwa?na je nikija kuanza mahusiano mengine mtoto atanionaje?
Wewe umeishi kwa uzinzi kwa miaka saba. Leo unajidai kuuliza utaishi vipi na mtoto uliyemzaa kwa njia ya haramu? mtoto yeyote anezaliwa nje ya ndoa ni mwana wa haramu. Mlee ki haramu haramu na umpachike baba asiye wake.
Pole sana dada @noella, Najua its so hard to raise a kid and most especially as a single mother.
Kwa kweli ladies labda niwashauri. If a man loves u enough lazima atatangaza ndoa! Achaneni na hao wanaume wengine wetu ambao wanaiponda ndoa takatifu na kusema wanajaribujaribu matokeo yake ni hayo mtoto then mnakuwa forced to live together then mara things are not working. Kwa nini tu usisubiri upendwe kwa haki na uzalie ndani ya ndoa?
Trust me ladies mwanaume hata akiwa player namna gani akikudondokea kisawasawa lazima atangaze ndoa ili asikukose na akumiliki kihalali....
Dada we tulia lea mwanao and there will come a man who will love you truly na utasahau kama uliwahi pata shida kwenye ndoa...Just pray, Mtoto atakuja elewa tu- kwani we ndo wa kwanza?
Jamani fungukeni rate ya watoto wanaolelewa na single parents Tanzania inaclimb sana!
Wapendwa, asanteni kwa michango yenu...
Japokuwa umeamua lakini naona kama sababu za kuachana ziko katika nafasi ya kurekebishika kama bado mapenzi yapo ya nini kumuhangaisha mtoto kiasi hicho?
Asanteni wapendwa kwa ushauri wenu,napata faraja ninapowasoma.
Cha kushangaza sasa hivi when am fed up with his behaviour yeye ndo anasema ananipenda,eti alikuwa hajui maana ya kupenda mpaka alivyouliza kwa rafiki zake. Nashukuru sana Mungu nimeweza kutoka kwenye haya mahusiano maana nimeteseka mno.
Wewe umeishi kwa uzinzi kwa miaka saba. Leo unajidai kuuliza utaishi vipi na mtoto uliyemzaa kwa njia ya haramu? mtoto yeyote anezaliwa nje ya ndoa ni mwana wa haramu. Mlee ki haramu haramu na umpachike baba asiye wake.
wamama wengi wanavumilia ukiritimba wa waume zao,ili watoto wao wakue....wewe kwa ukiburi wako,ukamuacha mume ulee peke yako...nani alikuambia usingle mother ni kazi rahisi?...mnh na huu mfumuko wa bei mbona you are in for it!......bora hata kwa wenzetu kuna schemes kibao za kuwasaidia single mothers,hivi kwani bongo hamna sheria ya kumbana mzazi atoe child suport pamoja na kutenga muda wazazi waliotengana waweze kumuona mtoto wao each....:thinking:
Eeeeh! Chonde chonde taratibu
wengi wao wamezoea kusikia mama zao wakilalamika,aah,mwanaume kitu gani? Mbona mi nimewalea mwenyewe? Na maneno mengine ya aina hiyo ambayo yana negative atitudes towards wanaume. Hivyo akiingia kwenye taasisi ya ndoa ukimkosea kidogo tu, anajua, ohooo..ndo wale wale! Hata kwa kosa ambalo ni la kurekebishana. Wengi wao ukikaa karibu nao utasikia kauli zao za kuonesha dharau kwa wanaume wakirefer kwamba mbona mama zao waliwalea peke yao hivyo mwanaume siyo chochote. Kuna wadada kama wawili nimesoma nao ambao nilikuwa karibu nao sana nilikuja gundua baadaye kwamba mama zao waliachana na baba zao na kuwalea wao as a single parent. Wana dharau mpaka hata we unayeongea nao muda mwingine unawakwepa.
Wewe umeishi kwa uzinzi kwa miaka saba. Leo unajidai kuuliza utaishi vipi na mtoto uliyemzaa kwa njia ya haramu? mtoto yeyote anezaliwa nje ya ndoa ni mwana wa haramu. Mlee ki haramu haramu na umpachike baba asiye wake.
wamama wengi wanavumilia ukiritimba wa waume zao,ili watoto wao wakue....wewe kwa ukiburi wako,ukamuacha mume ulee peke yako...nani alikuambia usingle mother ni kazi rahisi?...mnh na huu mfumuko wa bei mbona you are in for it!......bora hata kwa wenzetu kuna schemes kibao za kuwasaidia single mothers,hivi kwani bongo hamna sheria ya kumbana mzazi atoe child suport pamoja na kutenga muda wazazi waliotengana waweze kumuona mtoto wao each....:thinking:
Dada pole sana...
Situation kama hii iliwahi kumkuta mama nikiwa mdogo
na mama alichukua uamuzi kama wako na maisha yalisonga vizuri kabisa hata hata pale mama alipopata kuchumbiwa alinishirikisha na aliolewa na mtu mwingine na wanafurahia maisha
yao hadi leo na mimi namheshim
kabisa kama baba wa kunizaa
so usipoteze muda kabisa na huyo mshamba sababu he does nt respect your feelings.
Tulia then kuwa bussy na kutafuta
hela utapata anaekujali dada.
Mtoto wa nje ya ndoa, huwa "wazee waliofanya haramu" wanampa mateso. Kila ajae nyumbani anamwita "baba". Ukiuliza eti "utamaduni wa Kitanzania", hakuna utamaduni wa zinaa. Ni maadili kuporomoka.