Inapotokea tunataka kuvuka kwenda kwenye vijiji vya jirani au kama kuna mtu anakuja huku kwetu ni lazima wanaofanya hivyo wapite kwenye mto huo ambao hauna kivuko, maeneo mengi tumekuwa tukitumia mianzi kuvuka, jambo linalohatarisha maisha.
Nilibaini hivyo baada ya kuwa nimeondoka Kijijini hapo muda mrefu kwenda Dar kutafuta maisha, niliporejea ndipo nikaona hali hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imeniumiza sana na kunitafakarisha, inakuwaje ndugu zangu wanaishi katika maisha kama hayo.
Nilichoona na kunisikitisha wanatumia miti ya mianzi kuvuka, jambo ambalo ni hatari sana, kwani mianzi ni myepesi na ni rahisi kuteleza au kuvunjika inapokutana na uzito.
Nimefuatilia na kuambiwa na wenyeji zaidi yangu kuwa Watu kadhaa hupoteza maisha kila mwaka kwenye mto huo.
Suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko chochote, kutumia mianzi kuvuka mto ni kuweka maisha ya wengi rehani.
Wahusika watazame suala hili kwa uzito wake kwasababu linagusa maisha ya Watu, Mbunge wetu huku kwani hajui hiki kinachoendelea, viongozi wengine je nao wanasubiri nini au hawajui pia?