The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
?
Tunaweza kuona hali yetu ya nje kupitia muziki tunao usikiliza sio kuusikia, yaani maisha yametupa kusikiliza na kusikia. Je maisha yako yana usikiliza Muziki wa aina gani
Kuna baadhi ya nukuu za muziki zinazo elezea uwezo wa maisha ya kibinadamu ya sasa mfano Dizasta Vina anaposema " Nilimwambia Mama nitafuta yalio msibu na hata kama nitashindwa nitakufa nikijaribu" yule anaye usikiliza muziki huu anafunua kuishi kwa aina gani?
Muziki hufichua sauti zilizofichwa ndani ya moyo, Muziki hifichua ukweli na huulezea kwa maneno tuliyo yaficha yasisike. Maisha yako ya kimapambano yanausikiliza wimbo gani? maisha yako ya kimahusiano yana usikiliza wimbo gani?
Kuna wakati Muziki hutukumbusha ukweli hata kama tutahitaji tu kuupuuza kwa kusikia wimbo mwengine lakini ule tulio usikiliza na unao endana na maisha yetu utaendelea kupiga kichwani,hautaacha na kufanya ule tunao usikia ni kama kelele kwetu.
Tujiulize zaidi ni muziki gani tutasikiliza katika nyakati za dhoruba? ni muziki wa kishujaa, muziki wa huzuni kwakua muziki unao sikiliza una uwezo wa kukufanya kujificha ndani ya dhoruba au kutoka nje ya dhoruba 'a kukabiliana na dhoruba kupitia udhibiti wako
Rafiki wimbo wa maisha yako hautabadilisha maandishi yaliyomo ndani ya maisha yako, lakini hufungua njia tu ya jinsi ya kutoka au kushindwa kutoka kupitia nidhamu ya uidhinishaji wako.
Hivyo Muziki sio muunganiko wa maneno pekee bali ni ramani , na ni lugha pekee inayosikilizwa na nafsi yako .Unakuwa na muziki kila wakati, katika siku nzuri na mbaya, kila wakati kuna wimbo au msanii mmoja unayemsikiliza.
Ni ukweli kwamba katika muziki nyimbo tunazosikiliza na maneno tunayoimba yanaweza kutuathiri kwa njia kubwa. Na nyimbo hubadilika kila tunapoingia katika sura mpya ya maisha
Kila pigo la muziki huwasilisha jambo maishani,iki lipo pigo ambalo haliwasilishi jambo ni ukweli kuwa pigo hilo si kwa ajili yako.Muziki sio tu kuhusu kile tunachosikia, ni jinsi tunavyosikiliza, na jinsi tunavyokua katika tulicho sikiliza.
Hata sasa maisha yako yana usikiliza wimbo gani?