Maisha yalivyokua kabla ya Miamala

Maisha yalivyokua kabla ya Miamala

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Miaka ile ilikua ni habari za mdomo tu, unafahamishwa wafanya biashara wenye huduma ya kutuma pesa. Wengi walikua Kariakoo. Walifanya huduma hii katika mikoa yenye biashara zao.

Ukifika pale unatoa maelekezo ya ndugu yako aliye Arusha, jina lake na namba yake ya simu. Wanaandika katika daftari. Unaacha pesa unayotaka einde Arusha. Kwa kila transaction walichukua kama 2,000 ya vocha ya simu.

Kule Arusha utampigia ndugu yako simu, anakwenda dukani, au atapiga simu kwanza na kuwataarifu kuwa anakwenda. Akifika wanampa pesa ana saini daftari na kuondoka.

Ilijenga undugu na kuaminiana. Mara nyingi ukifika kama wamekuzoea utafanya na shopping ya mahitaji yako baada ya kukabishiwa mzigo wako. Wakijua unakaa mbali watakupa na chakula kabla hijaondoka. Na mkizoeana sana wanaweza kukupa pesa na ndugu yako akituma mnalipana.

Hii iliwasaidia wao kutokuzunguka na pesa ya biashara. Akifuata mahitaji ya duka Dar hela zinakua zipo Dar.

Baada ya miamala kuanza undugu na urafiki huu ulikufa. Ninadhani sasa ni wakati wa kufufuka upya.
 
Hiyo sikuwahi kuifahamu, naijua ile ya kutumia mabasi, unaenda kwenye ofisi zao na kitambulisho unasaini unachukua pesa. Baadae ikaja ya kutumiwa vocha, unatumiwa vocha za elfu 50 unaenda kuziuza kibanda cha simu hata kwa elfu 42. Tumetoka mbali.
 
Pesa unafuata posta enzi hizo.miaka ya 95 kushuka chini,mpaka kuna kitabu cha fasihi kwenye mitaala ya sekondari kiliitwa hawala ya fedha.usichanganye hawala na hawara
Kitabu ndo nakijua. 95 bado nilikuwa mdogo hiyo sikuifahamu.
 
Back
Top Bottom