Warumi wa kale ndiyo walikua wazalendo wa kweli. Katika jeshi wa Warumi kuanzia cheo cha Major kwenda juu ni lazima uwe Mrumi kwa kuzaliwa. Askari wa wa chini ya cheo cha Major walikua ni raises nchi wanayotawala.
Kazi ya Major kama hakuna vita ni kujenga miundo mbinu. Kuanzia barabara, kutandaza mabomba na kupump maji.
Jeshi la Warumi ndiyo lilianzisha mfumo wa pension. Askari walikatwa pesa kila mwezi itakayo wasaidia baada ya kustaafu. Na kuna kiinua mgongo cha mkupuo unalipwa baada ya kumaliza mkataba.
Maofisa wa jeshi walikipwa pesa iliyowatosha kununua ardhi na kuwekeza katika kilimo. Pia walimudu kujenga nyumba za kifahari.