stranger man
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 420
- 524
nimekaa nimefikiri Nini maana ya maisha na maisha yana Thaman gani Duniani? Ukitazama kwa haraka binadamu Nimtunaona maisha ya duniani yana thamani, Ni thamani gani ya maisha tunayoishi hata hatujui muda wa kuishi (life Span)?
Kuna haja gani ya kuvunjiana utu wa binadamu mwenzako kwa mambo ya maisha ambayo tunayalilia yawe mazuri iwe kwa njia halali au halamu? kuna haja gani ya kufanya dhuluma, wizi, mauwaji na vitisho kwa binadamu wenzako ambao inawezekana wakawa na Thaman sana kwa mungu Kuliko wewe
Nakumbuka kuna kitabu kimoja kinaitwa dunia uwanja wa fujo kilizungumza kwa ufupi dunia ni uwanja wa fujo kila mtu anafanya fujo zake na mwisho anaondoka zake.
simaanishi tusiyachukie maisha ya dunia, kwa sisi tulio masikini tuyapende na tufurahi mungu ametupa zawadi ya kuishi duniani tueneze upendo na vile vile tusaidiane.
Tujikite katika Kujenga thawabu kwa mungu tuache dhana ya kutafuta sifa ya kuacha mali duniani kwani vyote tulivikuta havitakuwa na thamani tena kwa mungu siku atakayotuita zawadi yetu kwake ni upendo na kuheshimu aliyoyasisitiza iwe ni kwenye Biblia au Quran.
Tusiishie kuwa na upendo kwa mungu upendo wa kweli uanze dunia pesa, dhahabu na magari ni mali za kupita nyumba yetu, tutarudi kwa huyu huyu tunaemkanyaga, tunechezea magari yake juu yake na tunae jenga maapartment mpaka karibu na mbingu si mwingine ni ardhi.
Nawatakia kila la Kheri Naomba kutoa hoja.