Maisha yanakwenda kasi sana. Juzi tu Polepole alikuwa kidume hapo Lumumba

Msukuma Original

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
928
Reaction score
3,330
Nikifikiria jinsi Mzee wa mavieite alivyokuwa na madharau na jinsi alivyokuwa anawapiga mkwara viongozi waandamizi wa CCM lakini leo hii naye anapigwa mkwara na Chongolo nabaki kujisemea tu dunia inazunguka.

Vijana ishini na watu wote kwa heshima na adabu, hakuna aijuae kesho yake. Polepole huyu alikuwa na jeuri ya kumkoromea yeyote kasoro JPM tu lakini leo amekuwa mdogo kama piriton.

Mwenye video ya Polepole akiwatambia watanzania kuwa anaendesha Vieite atuwekee please.
 
Waishi kwa heshima, adabu, hekima na kutumia akili,au kuchanganya na zao.
 
Wewe aliwahi kukudharau? Tusiwe Wepesi Kuhukumu Ilihali Nasi Tunamapungufu Kibao
 
Leo eti na yeye anapinga kupatiwa chanjo ya Corona kama Gwajima!! 😁😁😁 Ngoja aendelee kujifanya mkaidi! Yaani anapingana na msimamo wa Rais wake!! Angekuwa yule mwingine si angekubai faster tu kuchanjwa!!

Akitolewa kwenye ule ubunge wake wa viti maalum, VII YEITI ataishia tu kuiona ikipita barabarani kama sisi wenzake.
 
Hawo ni watu tu kama wengine wana mapungufu, huwezi kumrishisha kila mtu,hata hivyo ni nani ambae akipewa na madaraka atabaki vile vile kama alivyokua hana madaraka? Hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…