Maisha yananikatisha tamaa sana

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
1,984
Reaction score
3,695
Yaani basi tu, nimetafuta kazi sijapata, marafiki wamenikimbia, ndugu nao wapo kimya, hata nikiomba mtaji wananikatalia.

Nahisi kuchoka, nahisi kukata tamaa. Kuna muda nikilala natamani kusipambazuke. Sina baba, sina mama sina babu sina bibi. Muda mwingine naona hata waliopumzika makaburini wana afadhali.

kwanza nina umri wa miaka 26. Yaani nachoka kabisa😢😢😢
 
Mmh miaka 26 unalia lia kukosa ajira mbona mapema hiyo ni kama cooling break tu, kuna watu wana miaka 50 hawana mbele au nyuma ila kila siku wana damka kutafuta Rizki hawaja kata tamaa, we awamu ya pili ya mama ya 2025 hadi 2030, hutaiweza pesa ya Tz ina poromoka kwa kasi biashara zina kufa hamna ajira za serikali, bora ongea na wauza sumu ya mende panya wakusaidie tu .
 
Mkuu kama mzma afya unayo nguvu unayo na Bado unaishi kwa hilo tu mshukuru Mungu. changamoto kila mtu anapitia ili kujifunza kitu, ili cku unazifumania ufanye ya msingi maana wakati mwingine mali ukizipata kiraisi bila msoto zinaishiaga kwenye starehe tu. kaza buti fanya kama upo darasani vile unachukuwa kozi. One-day yes
 
Ubarikiwe sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…