Maisha yanapokufanya uonee wivu marehemu

Maisha yanapokufanya uonee wivu marehemu

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Wasalaam,

Jamani hali ya maisha imekua ngumu, kila kukicha mikosi.

Kila dili linafeli, ukiwa na shida marafiki wanakimbia, ukiomba msaada wanadhani unawakejeli hawakupi.

Ukiwaza kuroga upate pesa za ndago roho inasita maana umelelewa katika ukristo mpaka ndani ya moyo wako.
Nikijipa moyo nijichanganye na ndago picha za watoto Wangu na Mama yangu zinanijia kwamba ndago likikubali wanaweza wakawataka sadaka (kafala).

Ndipo nikiona mtu amefariki nashikwa na wivu na marehemu kwamba heri yake kaepuka balaa la dunia hi akapokee hesabu zake mbele huko.

Ewe Mungu nisamehe na tusaidie wazazi (hasa wanaume) tunaopenda familia zetu huku tunapitia changamoto ngumu za maisha hasa uchumi.
 
Heri wafu wafao katika Bwana tangu Sasa. Naan asema Roho wapate kupumzika baada ya tabu zao,kwa kuwa matendo yao yafuatana nao
 
Back
Top Bottom