Maisha yangekuwa rahisi sana kama wenye nyumba wangekuwa wanatulipisha pango per day

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
5,794
Reaction score
5,352
Mfano unalipa chumba elfu 30 kwa mwezi.

Inafika mwisho wa mwezi umejibana bana katika kipato/mshahara wako umebaki na tsh 20000(kuna watu wamecheka hapa)... Unafika kwa landlord anakuzingua anataka yote full ,atafoka, atajaza watu nk.. si kudhalilika huku

Ila wakikubali kila siku kupokea buku buku... Dah ingekuwa fresh aisee

Coz ni rahisi hata kama siku hiyo huna buku ukimfata mtu kama Mshana Jr ukimwambia nipe buku hapo... Anakupa fasta..

Ila una shida ya elfu 10 nani atakupa kirahisi rahisi... watu wenyewe kama akina Jane Lowassa au Mama Debora mmh
 
Lipa kodi mkuu kila kitu kina utaratibu wake wewe ukisema hvyo mwingine atataka katika hyo elfu moja ya siku awe analipa kwa saa kwa vigezo hvyo hvyo vya kwako
 
Kwa saa itakuwa usumbufu... bora kwa siku kila unavotoka azubuhi unamuachia cha kwake unaenda zako kwenye mishe zako... Au kila ukirud jion unamlipa chake kabisa then asubuh unasepa tu
 
Tumia akili kaka
Imagine umerud jion mweny nyumb anamuambia kesh mkabidh chumba chake? maan haun mkataba nae
Ndio maan Tunalip term ndefu ili uwe na aman kwa muda huo
 
unapewa mkataba kabla hujahamia mkuu.
mkataba unakueleza kabisa UNATAKIWA KULIPA TSH XXXX KILA SIKU,KUTO KULIPA FEDHA HIZO NI KIVUNJA MAKUBALIANO HAYA NA MWENYE NYUMBA NITAKUTOA NDUKI SIKU HIYO HIYO..

UNAKUBALI?
UNAKUBALI?
Weka tiki sehemu inayokufaa..

Nb, unaweza kulipa kwa mkupuo pia ukiweza.
 
Unaweza mbona wewe tafuta kibubu kila siku ukitoka unatoa hela ya watu mwisho wa mwez unampa kibubu chake mbona Simpo

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Hujawahi kukutana na shida mkuu.... Kuna siku nilichonga kibubu nikaweka ela asubuhi kufika saa 7 mchana nikavunja..nikatoa ile ile niloweka asubuh... Biashara ikaishia hapo
 
Kuna mama alipangishw flame ya biashar
Sas mweny flame alisem anatak hela yake kwa siku ambayo ni 10000 kwa mwez 300k
Baad ya kam miak miwil hv juzi yule mama akamwambia bhna mm nmepat mtu mwingin ko nikabdh flame yang
Imagine yul mpangaj hajajipang kw lolot

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
 
Unaiona buku ndogo sana eh mkuu? sikia nkusimulie hii...

Mwaka 2014-2015 nilikua nimepanga room Giza kabisa,kodi haikua ikinishinda ila changamoto yangu kubwa ilikua ni 300 zangu za kuchaji simu na tochi yangu kibandani,basi kwakua sikua na jinsi nikawa natoa tu zile 300.

siku moja nikiwa ktk mihangaiko yangu nikakutana na mawakala wa M-KOPA,walikua wanauza solar zao ambazo wanakupa set nzima ikiwa na panel,tochi,redio,na taa 4 kwa mkopo.

utaratibu wa kupewa n lazima utoe kianzio cha sh.40,000 kisha wanakupa kile ki solar chao,ambacho inatakiwa kila siku ili kitoe mwanga n lazima uweke M-PESA 1000,usipoweka 1000 m-pesa hata kama panel imepgwa na jua mchana kutwa betri lina charge "kitu hakiwaki".

basi nikawambia sawa buku hainishindi ntakua nalipa kila siku,utaratbu n uweke buku kila siku kwa muda wa mwaka mmoja kisha baada ya hapo mashine inakua yako na taa itawaka 24hrs.

Kufupisha story ni kwamba,baada ya kukabdhiwa ile mashine,nilimudu kukaa kwenye mwanga kwa muda wa wiki mbili tu,baada ya hapo nikashindwa nikawa nimerudi kwenye giza langu,nakaa tena baada ya siku kadhaa nikipata hela naweka buku umeme huo.

nataka kusema nini mkuu,Buku ni hela ndogo sana ukiisema na kuitamka na kuiandika lakini hii 1000 ukitaka kujua n mtihani na ni kubwa basi Zaa mtoto kisha kila siku iendayo kwa Mungu mpe mwanao 1000 ya kwenda nayo shule,halafu utaona kama hamna siku utakua unanuna ukskia dogo anagonga mlango anadai hela yake ya shule.

Shukuru Mungu sana utaratbu wa kulipa kodi kwa miezi 6 kwenda mbele,tena shukuru sana maana unakuokoa hata wewe hapo ulipo n basi tu hujaliona hilo,ila naamini ukikaa chini ukitulia Hutotaka utaratbu wa kodi kwa siku.
 
Maana yangu ni kwa hawa wamiliki waweke hii option ya kila siku.. Ila kama mpangaji siku mkeka umetema anaweza kulipa tu hata kifurushi cha wiki, mwezi au miezi.... Sio mwenye nyumba kulazimisha kuchukua pango ya miezi 3 au 6 n.k. eti kama huna hiyo ela chumba umekosa.

ndo kitu mi naona sio fair mkuu
 
Back
Top Bottom