Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Umuofia kwenu ndugu zangu
Kwanza ieleweke kuwa sipo hapa kujigamba wala kujipigia mstari, ni swali la kawaida tu nimelenga kuwashirikisha na kujifunza kwenu.
Ni kijana japo umri umesonga lakini sio kivile, elimu ya hapa na pale japo sioni kama naitumia moja kwa moja ila inaninufaisha na imesaidia kunichorea ramani ya maisha yangu.
Nilizaliwa na kukulia vijijini ndani ndani huko, ila baada ya kuonekana mwenye uwezo darasani na tabia njema, ikamshawishi ndugu mmoja kunivuta ili nikaishi na kusomea kwake.
Huyu ndugu ni babangu mkubwa ambaye alikuwa akiishi ‘mjini’ ukilinganisha na kwetu, ni mtumishi wa umma hivyo hata hali ya yake ilionekana ni maisha fulani ya kishua.
Kupitia baba huyu nikapata kuosha macho [exposure] na kujua upande mwingine wa dunia, mjini, na hivyo kujionea na kujifunza na kufurahia maisha mapya.
Hoja yangu iko hapa:
Pamoja na kile nilichokiona kuwa maisha mazuri na ya kisasa, lakini babangu huyu hakuwa na simu, nyumbani hakukuwa na TV japo ya chogo.
Makochi ya mbao na mito yalipamba sebule yakifunikwa vema na vitambaa, nyumba kubwa lakini madirisha hakuna nondo wala aluminiamu.
Hapo ni familia yenye kuheshimika baba na mama wote ni watumishi na mishahara inaingia, umri wao kipindi hicho ni kwenye miaka 45 hivi, kiufupi maisha yalikuwa mazuri kabisa.
Na hata ukiacha hapo, majirani pia na watumishi wengine sio kwamba walikuwa na maisha mazuri kuzidi... la hasha kote ilikuwa kama sawa tu na hata waliokuwa na TV basi ni chogo.
Sasa leo hii mimi katika miaka yangu 30 hii, japo sijajenga ila nalipa kodi nyumba ambayo ni bora kabisa, kodi ambayo siwezi kuwatajia wazee wangu hawa wataona nafuja pesa japo kwangu naona ni hadhi yangu.
Nimeweza kumiliki vitu vya thamani kiasi chake, hapa siongelei maTV makubwa na simu kali ila gari naogopa kurogwa [emoji16][emoji16][emoji16]
Na hapo sioni kama nimefika ila si haba kushukuru, yes naishi vema, maisha fulani ambayo wakinitembelea hawa wazee wangu ambao kwa sasa ni wastaafu wanahisi kupumzika.
Nina familia yangu, ndugu na wategemezi tumaini lao ni kwangu. Sijajenga wala sina gari lakini ramani yote ipo sawa ni suala la utekelezaji tu, InshaAllah.
Sasa nilichojiuliza ni kama hivi, ni nyakati tu zimebadilika na imekuwa kawaida kumiliki hivi vitu, au ni kweli nipo kwenye ‘raiti traki’ kuyaelekea mafanikio?
Wazee wetu walioishi na kusota hadi hadi kustaafu ndo wanajenga, ni kwa sababu ya nyakati au ni kweli maisha yalikuwa magumu.?
Sijui kama nimeeleweka, nitarudi, acha nijifukize kwanza.