SoC04 Maisha yangu yalianza kuwa magumu baada tu ya kutaka kuwa mtu mzuri kwa kila mtu

SoC04 Maisha yangu yalianza kuwa magumu baada tu ya kutaka kuwa mtu mzuri kwa kila mtu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Leticia shija

New Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Nimewahi kukutana na msemo mmoja unasema "Maisha yangu yalianza kuwa magumu baada tu ya kutaka kuwa mtu mzuri kwa kila mtu".

Kwenye haya maisha unaweza ukawa mtu mwema tu lakini ikawa si lazima kuwa mtu mzuri kwa kila mmoja. Watu wengi wanajitahidi sana kuwa watu wazuri au waonekane kuwa wao ni watu wazuri kwa kila mtu na mwisho wao wanaishia kulia na kufedheheka. Kitu kingine unachopaswa kujua kuhusu watu ni kwamba Usijishushe sana kiasi cha kuondoa utu na thamani yako.

Alafu, katika yote unayoyafanya usisahau kwamba wewe ni Brand, usijisogeze sana kwenye maisha ya watu ilihali hawakutaki na kuna muda wakikuhitaji utajitokeza lakini wewe ukiwahitaji hawata jitokeza hata tu kukusaidia jambo dogo, watu wana watu wao.

Weka misimamo yako thabiti kabisa kwenye maisha yako, waoneshe watu mipaka yako kwenye maisha yako. Kitu cha mwisho kabisa na cha msingi usiruhusu watu wakujue sana, wape watu machache wanayopaswa kujua kuhusu wewe mengine Baki nayo Rohoni na moyoni mwako
 
Upvote 1
Weka misimamo yako thabiti kabisa kwenye maisha yako, waoneshe watu mipaka yako kwenye maisha yako
Hakikisha tu imeegemea kwenye ukweli kwerikweri hiyo misimamo. Tunaishi kujifunza, sasa ukisimamia tu msimamo na kuzikataa data na taarifa mpya zinazopingana hatutaendelea
 
Back
Top Bottom