Maiti zichomwe Moto kuwe na Vikaburi vidogo au Majivu yatupwe Baharini.

Guru Master

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2017
Posts
226
Reaction score
594
Kufa ni mara moja tu na ukishakufa unaoza then you are done. Hamna jingine tu juu ya mwili wako. Tusipoteze pesa nyingi na kuingia gharama kumzika mtu ambaye ktk ulimwengu huu ashapoteza uwepo wake.

Ni aibu watu wanapogombea maiti. Huwakuti hawa wakigombea kuuguza. Linapokuja suala la kuuguza huwa watu wanakuwa mbali sana. Ila hupenda kuonesha umuhimu wakati wa kuzika.

Kama mtu amefariki matendo yake ndiyo yatakayomfuata. Azikwe panapowezekana ama sivyo kama ana sehemu maalumu ya kutaka kuzikwa asisahau kuacha na pesa.

SIyo mtu akiwa hai anasema akifa akazikwe Mwanza. Halafu kaondoka hajaacha nauli au pesa za kusafirisha maiti kwenda Mwanza. Ni vyema akasema kama anataka akazikwe Rukwa na sasa yeye yupo Dar aache kabisa pesa ya gharama za kusafirisha.

Na kama anaumwa basi ni vyema akajongea kabisa eneo la tukio ili afie huko. Siyo analazimisha kukaa town mpaka ana pass away then anataka akazikwe Mkoani huko Mbali na hakuacha pesa kwa ajili hiyo.

Otherwise. Maiti zichomwe moto majivu yasafirishwe. Au maiti zizikwe pale panapowezekana
 
Atatokea mwingine atasema kuchoma ni gharama bora atoswe baharini, mtoni au ziwani.
 
Nikifa mkanichoma moto majivu mkatupa baharini...YESU akija kutufufua siku ya mwsho..sitaweza kuogelea..MAANA SIJUI KUOGELEA
 
Hapo itakuwa sawa na kupoteza kabisa ushahidi wa kibaiolojia (forensic analysis) endapo itakuwepo tashwishi kwenye kifo cha mtu fulani. Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Palestina, Yasir Arafat ulipofukuliwa kwa oda ya mahakama, ilibainika kwamba alikufa kwa sumu ya poloniamu, tofauti na maelezo ya maghumashi ya awali. And that changed almost everything.
 
Unataka tukitaka kufufuka tushindwe?
Ila watu mna roho mbaya sana.
 
Mafundisho ya kiislamu yapo hivi

Kaburi halitakiwi kujengewa kwaio mnaweza kuja kuzika tena baada ya miaka kadhaa na hpo ndo tunaona kua Uislamu ulishayaona haya mapemaa
Ardhi ni ndogo asilimia kubwa ya dunia ni maji sasa ndo mna Allah na mtume wake wakatufundisha hivo.

N.b.Wapo waislamu walojengea makaburi lkn sheria ya kiislamu inakataa jambo hilo
 
Yeah!
Nakubaliana na hoja kwa sababu mambo yamekua rahisi sana, unakata bima ya maisha basi wala hakuna mambo ya michango kukodi noah kukupeleka manyovu ndanindani.
Natofautiana na kupoteza kumbukumbu ya kizazi lazima family tree izingatiwe
 
Unataka tukitaka kufufuka tushindwe?
Ila watu mna roho mbaya sana.
Ukute majibu kayatapanya mlagarasi indian ruvu victoria na tanganyika lengo mpaka ufufuke tayari jina lako lishaitwa na jibril kashasepa😂😂
 
Mmh hii land tuliyonayo Afrika bado tuna ubahili wa kumiliki ardhi ya kuzikia!
Mazishi ya kifahari ya kutumia saruji na vigae ni uharibifu mkubwa sana wa mazingira.

Kama kuzika ni jambo la heri, basi iandaliwe sheria ili mazishi yote yafanyike simple kama wanavyozika waislam.

Pasiwepo vikorombweso hatarishi vya kuharibu mazingira ili ardhi husika iweze kutumiwa tena baadaye.

Kuchoma maiti na kwenda kumwaga majivu baharini ama kuyazika ni njia sahihi ya kuhifadhi mazingira.

Wenye imani zao za kufufuka, waelewe kuwa Mungu atawafufua popote walipopotezea maisha kwa namna atakavyoona inafaa.

Wajiulize na wafikirie namna ya ufufuko wa wenzao wanaokufa kwa kumezwa ama kuliwa ama kuteketea kabisa bila kuzikwa.
 
Kwani wakinunua vigae wanakukopa helazako na wanashindwa kuzirudisha?
 
Back
Top Bottom