Majaji wanapatikana kwa mchakato gani Tanzania?

Majaji wanapatikana kwa mchakato gani Tanzania?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tanzania Majaji wanapatikanaje? Au Rais anaweza akamteua mtu yeyote kuwa Jaji? Sioni kama kuna mchakato wowote unaoihusisha mahakama kuwapata majaji.

Naona kama serikali ndio walioshika nyenzo zote za majaji na ndio maana kadri siku zinavyokwenda idadi ya majaji wasiotokana na mfumo wa mahakama inaongezeka Jambo linalokwamisha upatikanaji wa majaji wenye uzoefu.

Mtu anatoka kumiliki ofisi ya uwakili Hadi Jaji, au anatoka kwenye uendesha mashtaka hadi Jaji? Je, ni sahihi nafasi ya ujaji ikiwa sehemu yakwenda kufanyia majaribio?

Hakuna usahili
 
Kamanda Beatrice naona weye ni mfuasi wa "wenzetu" Kenya, au tuseme wenzenu: kazi za Jaji hutangazwa magazetini na kupeleka maombi ya ajira kama vile unaomba Uhasibu. System yetu ya majaji ni tried and tested, inafuata katiba (with regard to separation of duties), lakini inafuata miiko ya utumishi (Executive).

Rais kwa vile ndiye Mbunge na muwakilishi wa kila mtu (hakuna mwingine kama yeye) anapewa madaraka makubwa - and quite rightly so - kwa niaba ya waliomchagua. Kana Rais ni wa CCM, sawa tu, ndiye waliyemchagua. Kama atawapendelea wenye mawazo kama yake, sawa tu, nyani hutamuona anatembelea kuku.

Hivi hushangai wenzenu Kenya kumuona Mbunge Orengo ndiye advocate wa Yuda Raila mgombea, sawa na Dr Tulia amtetee tundulissu? Kenya ni idiots, hawana kabisa separation ya Judiciary na Legislature, wala hawana cha kutufundisha.
 
Kamanda Beatrice naona weye ni mfuasi wa "wenzetu" Kenya, au tuseme wenzenu: kazi za Jaji hutangazwa magazetini na kupeleka maombi ya ajira kama vile unaomba Uhasibu. System yetu ya majaji ni tried and tested, inafuata katiba (with regard to separation of duties), lakini inafuata miiko ya utumishi (Executive)...
Kwa maana ya kuwa kwetu tuna utaratibu mzuri zaidi ambao kwa mujibu wa katiba, rais huangalia tu vichwa vya watu yaani "head hunting?"

Hiiiiii bagosha!
 
Tanzania Majaji wanapatikanaje? Au Rais anaweza akamteua mtu yeyote kuwa Jaji? Sioni Kama Kuna mchakato wowote unaoihusisha mahakama kuwapata majaji...
inategemea tu unamjua nani, umeoa wapi, mkweo anakuunganisha, au rafiki yako yuko close na mtu fulani unapigiwa connection basi unakuwa jaji unakula maisha.
 
Tafuta ile hotuba ya jaji mkuu wakati wa kuwaapisha majaji wa mahakama kuu na ya rufani hawa wapya kina ex dpp
 
Kamanda Beatrice naona weye ni mfuasi wa "wenzetu" Kenya, au tuseme wenzenu: kazi za Jaji hutangazwa magazetini na kupeleka maombi ya ajira kama vile unaomba Uhasibu. System yetu ya majaji ni tried and tested, inafuata katiba (with regard to separation of duties), lakini inafuata miiko ya utumishi (Executive)...
Ndiyo maana Kenya wameendelea sisi tuna rudi nyuma kila siku mahakama zimegeuzwa kuwa matawi ya CCM
 
Back
Top Bottom