Majaliwa apandishwe awe M/Rais, Mwigulu awe W/Mkuu au Nchimbi awe M/Rais, Mwigulu awe W/Mkuu

Majaliwa apandishwe awe M/Rais, Mwigulu awe W/Mkuu au Nchimbi awe M/Rais, Mwigulu awe W/Mkuu

Automata

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2015
Posts
3,414
Reaction score
4,794
Nchi kubwa ya Tanzania si nyepesi; serikalini si kwepesi, chamani si kwepesi, na uraiani si kwepesi

Kwa hiyo Mh. SSH anatakiwa kuwa na wasaidizi very bold 'strong'

  1. Wanaoijua siasa
  2. Wanaokijua chama
  3. Wanaoijua serikali (ki muundo, mfumo na taratibu)
  4. Wanaowajua na watakao wamudu watanganyika wenzao ambao huwa na sifa za ubishi, utemi, mfumo dume, upigaji (wizi, rushwa na ufisadi), nk.
  5. Bila kusahau sifa za msingi za uzalendo, bidii ya kazi, ubunifu, na nk.

Option 1
VP - Majaliwa
PM - Mwigulu

Option 2
VP - Nchimbi
PM - Mwigulu

Sifa zao 'kibinafsi'
Majaliwa - yeye pamoja na Mh. SSH walikuwa wasaidizi wa juu kabisa wa mzee, pia alizunguka kuinadi ilani, kwa hiyo naye pia anajua vilivyo mipango na matarajio ya mzee (watasaidiana kuikamilisha)

Mwigulu - amehudumu chamani na serikalini (kama mtumishi wa uma na kiongozi kupitia nafasi za kisiasa), ni mdogo kiumri kwa Mh. SSH kwa hiyo anafaa kutumwa tumwa (leo Mara, kesho Mbeya, kesho kutwa Arusha)

Nchimbi - amehudumu chamani na serikalini, na kwenye nyanja za kimataifa 'kama balozi', naye pia ni mdogo kiumri kwa Mh. SSH
 
Mwigulu katika medani za siasa za kimataifa yupoje kwanza? Tuanzie hapo tukimalizana na huyo tuje kwa majaliwa sasa.

(hapa nitaomba ka video kafupi akimwaga ung'eng'e japo hili sio swala la msingi kwenye mambo ya kizalendo hata baafhi ya viongozi wa uchina hawajui kizungu ila ndio hivyo taifa kubwa)
 
VP hawezi kuwa miongoni mwa wenye majimbo. Wawatumikie watu wao kwanza tutawaangalia 2025
 
Ramli Chonganishi
Manyaunyau!!😥😣🙄😶😑😐☺🙂😎
 
Bandiko limewafanya Majaliwa na Nchimbi kama option
Mwigulu ni compulsory

Ukikatiza huko kwenye barabara za kwenda mikoani utaona matangazo ya Mwigulu ndio raisi ajae

Tunaweza kuwa hatuoni vizuri lkn si kwa Mwigulu

Rudi kamwambie hatujawa vilaza sana,wachapakazi tunawajua

Atatuuza mapema asubuhi


Sijaona kama ana hadhi
 
..Mwigulu ana historia ya kuwa na siasa za hovyo.

..kwasababu Rais Samia ameamua kufungua ukurasa mpya basi siyo busara akateua wasaidizi waliohusika na siasa za hovyo wakati wa utawala wa JK na JPM
 
Ningekuwa mimi ndio SSH Vp wangu ningemchangua William Lukuvi na Vp wangu awe Profesa Ibrahim Juma Assad CAG Mstaafu
 
Katiba inamtema majaliwa kuwa VP na mwigulu pia....hawaruhusiwi kwa vile ni wabunge
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom