Majaliwa: Kampeni ya 'Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja' inaenda kupunguza pengo baina familia zenye uwezo na zisizo na uwezo

Majaliwa: Kampeni ya 'Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja' inaenda kupunguza pengo baina familia zenye uwezo na zisizo na uwezo

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Kauli mbiu ya 'Kitabu Kimoja Mwanafunzi Mmoja' itasaidia kukuza usawa kwa kupunguza pengo baina ya familia zenye uwezo na ambazo hazina uwezo.

Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo ambayo yamefanyika leo March 7, 2025, amesema kuwa TET wamekuja na kauli mbiu ambayo inalenga kuwezesha upatikanaji wa vitabu mashuleni kwa kila Mwanafunzi kuwa na kitabu kimoja kwenye kila somo.

"Kauli mbiu hii inasaidia kupunguza pengo elimu kati ya familia yenye uwezo na zile ambazo hazina uwezo, kwa sababu sasa kila Mwanafunzi atapata Kitabu chake katika kila somo"amesema Waziri Mkuu

Ameongeza kuwa suala hilo likifanikiwa kutekelezeka litawezesha vijana kupata elimu sawa na pia kuchochea hamasa ya Wanafunzi kusoma zaidi.

Aidha ametoa wito kwa taasisi hiyo kuongeza ubunifu zaidi katika kutafuta rasilimali fedha kwa kiwango ambacho wamelenga ambacho ni Bilioni 297, ambapo ameshauri waendelee kutengeneza matukio ya kuwaleta pamoja wadau ili kuweza kuchangia.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Anselmo Komba ameeleza kwa ufupi mafanikio ambayo taasisi hiyo imepata, ambapo amesema kwamba wamefanikiwa kuongeza wanataaluma wenye ngazi za juu katika elimu, kuanza kutumia mifumo ya kidigitali ikiwemo kuanzishwa kwa maktaba ya mtandao ambayo uwezesha Wanafunzi kujisomea wenyewe.

Utaratibu ambao uliwekwa wazi ili wadau waweze kuchangia kampeni ya kitabu Kimoja kwa Mwanafunzi Mmoja' ni kwa kutumia namba ya malipo ya serikali ambayo ni 994040118259. Ambapo Kampeni hiyo ni endelevu mpaka siku ya kilele cha maadhimisho hayo Mwezi Juni, 2025.
 
kwa nini ukifika uchaguzi wazari mkuu na wabunge ufanana rushwa za kutaka kufikia serikalini
 
Back
Top Bottom