Uchaguzi 2020 Majaliwa: Tusimchague mtu kwakuwa amepanda jukwaani kwa mbwembwe, lazima tupate Kiongozi atakayeweza kutuunganisha Watanzania wote

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema wananchi wanatakiwa watafakari kwa kina wakati wanapochagua kiongozi kwa kuwa uongozi wa nchi si jambo la mzaha wala la majaribio ni lazima apatikane mtu makini atakayeweza kuwaletea maendeleo.

“Lazima tujue historia yake kiutumishi tusimchague mtu kwa kuwa amepanda kwenye jukwaa kwa mbwembwe, lazima tupate kiongozi atakayeweza kutuunganisha Watanzania wote na atakayetunza amani. Lazima tupate kiongozi atakayewasaidia wanyonge naye ni Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea urais kwa tiketi ya CCM.”

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 9, 2020) alipozungumza na wananchi wa jimbo la Mlalo wilayani Lushoto, Tanga katika mkutano ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt Magufuli, mgombea ubunge jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi na wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wote wawachague wagombea wa CCM katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani kwa sababu wanatoka katika taasisi yenye uwezo wa kuwatumikia wananchi wote bila ya kujali itikadi za aina yoyote. Amesema viongozi hao watakwenda hadi vijijini na kuwatumikia kupitia Ilani.

Mheshimiwa Majaliwa amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu na kwenda kumchagua Dkt. Magufuli katika nafasi ya urais kwa sababu tayari wameshuhudia kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. “Tukamchague Dkt. Magufuli aendelee kusambaza maendeleo.”

Amesema maendeleo hayana chama hivyo wananchi wote bila ya kujali itikadi za vyama vyao wahamasishane kwenda kumchagua Dkt. Magufuli ambaye ni kiongozi atakayeweza kushirikiana nao vizuri katika kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao kwa kutumia Ilani ya uchaguzi ya CCM, ambayo imeanisha kila kitu.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa nishati ya umeme Mheshimiwa Majaliwa amewahakikishia wananchi hao kwamba vijiji vyote 85 katika wilaya hiyo ambavyo bado havijafikiwa na nishati ya umeme vitafikiwa. Wilaya hiyo ina vijiji 208 kati yake vijiji 123 tayari vimeshaunganishiwa umeme.

Amesema Rais Dkt. Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Lushoto. Gharama za kuunganishiwa umeme huo amezipunguza kutoka sh. 380,000 hadi sh. 27,000 tu.

Pia Mheshimiwa Majaliwa amesema wananchi hawatowajibika tena kulipia gharama za nguzo wala hawatalipia fomu za maombi ya kuunganishiwa huduma hiyo ya umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zote zimeshabebwa na Serikali yao.
 
Hii ndio kampeni ya Tanzania...
Hatari sana
 

Anayetuunganisha wote ni yupi?

"Msichague watu fulani hata kama wanafaa"
"Mchagueni huyu asiyesoma kwa kuwa ninaweza kufanya naye".
"Msiponichagua siwaletei maendeleo hata kama mnalipa kodi"
"Mkurugenzi atakayetangaza washindi wa kambi nyingine ...... hata kama wamechanguliwa"

Huku kuunganishwa ni kupi?
 
Asante, huyu aliyepo hawapendi wapinzani kama unavyomshuhudia kwenye mikutano yake, hivi sasa watanzania tumegawanyika kuliko wakati wa ukoloni! Pia anawabagua wanawake kama kaulizake zinavyosikika kwenye mikutano yake.
 
Angekuwa yeye ni mtunza amani kweli, atufahamishe alipo Bensaanane?

Atufahamishe pia alipo mwandishi wa habari, Azory Gwanda?

Atufahamishe pia ni kina nani walimminia risasi zaidi ya 15 kwenye gari lake, Tundu Lissu, zaidi ya miaka 3 iliyopita, ambapo hadi Leo, hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na kuhojiwa?

Hizo ni siasa tu, kwani siyo kweli kuwa Magu ndiye atatunza amani ya nchi, Bali yeye ni chanzo cha kuitowesha amani ya nchi hii!
 
Huyu anayoongeaga haya hapati kura yangu
 
Lisu atosha
 
Msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert
 
Unajaribu kupalilia kuupata tena uwaziri mkuu.Jimboni kwako wewe ni viti maalumu na ulifanya hivyo kwa makusudi ili upate nafasi ya kuzurura nchi nzima kuomba kura kwa mtu watanzania wasio mtakaa tena.
 
Kwa hiyo anamsimanga bosi wake?maana yeye ndiye anapanda kwenye majukwaa kwa mbwembwe na waigizaji wake
 
Huu upuuzi wa kusema maendeleo hayana chama sijui wanautolea wapi. Uhwezi kusema hivyo halafu unatuambia ukitaka maendeleo changua CCM. Yaani hawa watu wanatuona sisi mafala kupitiliza. Kura yangu itakwenda kwa ....
 
Majailiwa amepiga dongo zuri sana linahitaji akili kwa mbaali kidoooogo na ufahamu wa kuzaliwa,japo amechomekea kinaitwa kibwagizo hakuna isipokuwa Magufuli.

Kwa alipo hawezi moja kwa moja kuwataka wananchi wasiichague tena, tumemuelewa CCM haichaguliwi tena.
 
yes hatutaki mtu aliyepanda jukwaani kwa mbwembwe za wasanii na kupiga magoti.
 
"Chagueni chadema" maendeleo hayana chama.
 
Vipi zile "push up" safari hii zimeishia wapi? nasikia siku hizi badala ya "push up" msafara wake unaongozwa na ambulance, kweli maisha yanabadilika upesi sana.
Alijiona mwamba kuliko Mungu huku hajui nguvu ya mwili inategemea hisani ya Mungu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…