Leo Waziri Mkuu alivyokuwa Lamadi akielekea Bunda ameongea maneno mazito sana kuwa Serikali ya JPM imenuia kuhakikisha kila kaya ina umeme
Iwe ya nyasi tembe mbavu za mbwa zote zitawekewa umeme na kama nguzo hazifiki mfano visiwani watafungiwa sola hukohuko, hakuna kutumia kibatali wala koroboi wala chemli wala karabai hizi zote zitakuwa zana za kale zitapelekwa makumbusho ya taifa kama kumbukumbu.
Kaka Kasim kaagiza nguzo zigawiwe bure, tena zigawiwe ka njugu, hata kama uko nyuma ya mlima nguzo itakufuata hukohuko,
Kwa wapenzi wa kufugafuga kuku bata si ndio neema hii kule shambani kwangu nitaweka na mabanda ya kuku kabisa umeme upo.
JPM hapa masikini katukomboa kwelikweli, namie najitolea laki wahitaji watano wawekewe umeme nao.
Ndio maana alisisitiza bwawa la nyerere lijengwe haraka kumbe tusijekosa umeme maana mambo ya mgao hataki kabisa kusikia.