Majambazi wavamia nyumba ya Q Chillah, waiba vitu vya zaidi ya milioni 2

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Q Chila amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.

Akiongea na Clouds FM, muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni kama milioni mbili au tatu.

“Watumishi wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama sita, saba au nane.

Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila kitu?,” ameuliza Q Chila.

“Pale sebuleni mavitu mengine yote wamepita nayo na gym ya nondo ilikuwa tulichukua Mlimani kwa sababu ya exercise,” ameongeza.

“Wamepiga maplazma, wamepiga music system yangu nimetoka nayo South Africa, wamepiga laptop ambayo tayari mimi nilikuwa naangalia nafasi ya kujipanga na connection zangu.

Wamepiga piga hivi kama tatu point something au mbili point something wamepiga,” aliongeza.
 
Hao ni vibaka sio majambazi. Yani unaamini kuna jambazi karne hii anaiba tv au furniture?
 
"Q Chila amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake."

Mungu awalaani na wala wasipate mafanikio yoyote huko waendako
 
What goes around comes around , Q chief alikua mpigaji sana na yeye kitambo vifaa vya magari , kwenye show za q chief ilikua lazima magari zaidi ya 20 , show ikiisha yameibiwa alikua na kundi lake acha wampige na yeye unaweza ukakuta no hao washikaji zake wa zamani vibaka kawatosa ndo wanamkomesha
 
Leta ushahid
 
Jambazi haji kupiga ramli (kubahatisha) na akiingia kafata pesa,sio hizo takataka alizozitaja na ana uhakika pesa ipo na sio hela ya kununulia karanga.
 
Mwizi(labda kastaafu) nae hua anaibiwa???
 
Pole Ndg Q-Chillah
Mapolisi wetu wapo busy na mazoezi ya UKUTA mabarabarani wakati majambazi yanaendelea na mambo yao.
 

hawa wasanii wanatafutaga kiki yakutolea nyimbo alikiba nae alisema amevamiwa picha alizopost sikuzielew baada ya mda kidogp tukasikia anatoa nyimbo lakini natoa pole kama kweli ameibiw na hao vibaka
 
Pole sana Chillah! Nimejikuta naimba ule wimbo wake "Ungeniumiza" #macho yalinidanganya mbele sikuona..nikajikuta nampenda sanaa..,bila kujuaa..mbele ungeniumizaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…