QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu amesema kuwa endapo atachaguliwa tena ataanzisha mpango maalum wa kuwakopesha zana wavuvi katika maziwa ya Tanzania.
Aidha, Rais Kikwete amewatangazia majambazi wanaofanya uharifu, kushambulia na hata kuua wavuvi katika maziwa ya Tanzania kuwa sasa kiama chao kimefika.
Rais Kikwete ameyatangaza hayo siku ya Jumapili, Septemba 26, 2010, wakati alipofanya mikutano ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu katika maeneo ya Busekera, Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara; na Ukara, Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza.
Kwanini haya hayakufanyika tangu mwaka 1961, yamekumbukwa mwaka huu? CCM chama kikongwe kilikuwa wapi muda huo wote?