Majambazi yauwawa Sinza

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Habari za asbh, leo hii nilipita pale Sinza ofisi za TRA saa kumi kamili baada ya dk 2 kulipita lile jengo nilisikia mirindimo ya RISASI polisi wakitunukiana na majambazi kama wengi wenu mngefanya nilikiingiza kistarlet changu katikati ya nyumba za watu kuokoa roho yangu na huku wengine wakipaki na kuacha magari pembeni ya barabara na kukimbia. Baada ya muda nikapita tena na kukuta jambazi moja limelala pale chini na askari wakilizunguka. Mwenye data zaidi tuhabarisheni..
 
Sasa majambazi yauwa au yauwawa ?
 
Yauwawa kaka kumradhi maandishi.....
 
Yauwawa kaka kumradhi maandishi.....

Ndio maana yake, kwani kulikuta jambazi limelala vilevile umeniwacha njia panda.Na ulikuwepo kwenye scene,hivyo nilikuwa na tamaa kwamba wewe ndio utakaekuwa na data kamili ,kwa ufupi hata kile walichotaka kufanya majambazi hao kingekuwa kinazungumzwa hapo.Na wewe ambae ulikuwepo live ni bahati kwa JF !
 
Yauwawa kaka kumradhi maandishi.....

Kama umerekebisha na kuwa "yauwawa", sasa swali lingine, ni majambazi au jambazi? Rekebisha tena halafu useme kumradhi maandishi kwa mara nyingine.
 
Na je kama aliyeuwawa ni mwanachi mpita njia tu asiyekuwa na hatia yoyote? Maana hili pia lawezekana.
 

Predeshe, nadhani wewe ndiye haswa wa kuihabarisha JF...hiyo simens yako haina hata camera? wakati unapaki starlet yako ungeweza chukua picha habari hii ingependeza zaidi.
 
Na je kama aliyeuwawa ni mwanachi mpita njia tu asiyekuwa na hatia yoyote? Maana hili pia lawezekana.

Aka, mie wala sikuwepo eneo hilo lol
Anyway, hivi ofisi za TRA zipo Sinza au Mwenge?
lakini inaonekana kuwa hawa bandugu wanaanza kurejea tena kwa nguvu. Walianza pale magomeni petrol station, wakafanyiza Manzese, na sasa hili tena. mwema na vijana wake wanapaswa kukaza buti kwa sababu tulishaanza kusahau matukio haya
 
.....Jamani huyu ni Pedesheeeeeeee .. kawambieni alitoma maskani kwa watu na starlet yake kusevu maisha yake ..sasa angewezaje chukua picha, hope zingezidi kuunguruma hata starlet angeiacha barabarani usipime mlio wa shaba vijana wakazi wakiwa wanafanya forced 'income distribution' mwanawane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…