Majanga UDSM:Zaidi ya wanafunzi 500 wamedisco katika mwaka wa masomo 2012/13

Unaelewa tofauti ya kushikwa na kudisco?
Idadi hiyo ni kubwa sana kwa disco, poleni wahanga.
Tatizo sidhani kama ni wakufunzi, maana hawajaanza kazi leo.
Tatizo ni misingi mibovu ya elimu za vijana wetu wa sasa, pamoja na anasa

mkuu kuna hii course inaitwa CL106,jamaa walikua wanasema watashika watu idadi ya shato 5 za mabibo na 5 za cumpus,na kweli wametimiza dhamira yao.
 
Mkuu mwambie na wengine wananunua mitihani,
 
Ndo masuala ya Consultation hayo.

Watu wako bussy na kupiga noti kufundisha ni kama wanazuga tu,na lisipoangaliwa kwa ukaribu litaendelea kutafuna elimu ya juu mpaka mtalia machozi ya damu
 
500 ni kidogo sana kwa idadi ya wanafunzi kwa miaka yote!walimu wamekua fair sana

nimesikia hata prof mkandala amejitapa eti anasema mwaka huu vijana wake wamejitahdi kuwa seriouz na shule.sasa cjui miaka ya nyuma walikua wanadisco idadi gani?
 
Hiyo ni idadi ya kawaida sana kwa UDSM. Hata hivyo nimeshangaa eti school ya sheria wamedisco 42 tu? Tulizoea kuona disco hadi 200 huko, school of Education disco kama 70 hivi, na kule school of science disco nusu ya darasa wanadisco. Lakini naona kwenye disco zilizopo hapo ni engineering tu ndiyo wameumia zaidi.
Lakini nafikiri kuna haja ya kuangalia upya utaratibu wa ufundishaji na utoaji wa mitihani. Kuwadisco maengineer wengi kiasi hiki, ni hasara sana kwa taifa letu.
 

Mkuu nimemkumbuka ngowi the jargon
 

kuna lipi la kushangaa hapa, kama hawakuwa name msingi mzuri unatarajia nini? tatizo no mfumo uliopo mbaya hata walimu ni failures, kwa upande Wa pili tujiulize kwamba, ni kweli walikuwa wanasomaa?au walikuwa muda mwingi wanapiga umbeya kwenye mitandaooo?
 
Wahitimu wengi wa UDSM tuko nao mitaani.Uwezo wao kwenye fani unatia shaka kulingana vyeti vyao. Kwa mwendo huu ni vigumu kushindana kwenye soko la ajira Afrika Mashariki.
 

Kweli kabisa kuna watu wengi wanapoint nzuri ila hawajiwezi hasa wanaotoka kwenye Seminary za kutafuniwa, kuna watu wametoka kwenye shule za kata na Div. III zao wanaperform vizuri zaidi kwa kuwa wameshazoea kujihangaikia wenyewe. Na chuo bila kuhangaika mwenyewe library utapata shida na ukitoka utakuwa kilaza tu
 
Na kuna watu hawajaziwea uhuru wa chuo, kwamba maamuzi yote unayo mwenyewe ila mtakutana kwenye mtihani. Sasa wa geti kali akishaingia mazingira hayo, anakuwa kama vile ndo anabalehe, full genye mshindo, full kujirusha na full kitegemea kudesa na matokeo yake ndo huwa hayo

kuna wati bumu kama halijaisha hawawezi kusoma na wakiishiwa hapasomeki tena
 
hivi hawa wanaoishia katikati ya njia nao wanatakiwa kulipa ile mikopo?
 
Hamna kitu, haya ni maneno ya mkosaji tu! Wanafunzi someni acheni mzaha.....!
 
washapishanj na bumu haoo
waendelee kuwachangia watanzania wenze
 
au maoni yaliyotolewa juu ya degree ya naibu katibu mkuu mmoja yamewatia mashaka na kuamua kuwa serious ili kuwabana wale wanaopata 'grade 1' fake!?
 
Tatizo la kuchagua vyuo via TCU ndo hili sasa maana zamani walikuwa wanachuja watu wenye vigezo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…