Majanga yaliyonikuta jeshini

Majanga yaliyonikuta jeshini

Al-Hadidy

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
1,411
Reaction score
3,077
Miezi mitatu niliiona kama mwaka ilikuwa ni majanga tena si ya nchi hii
1-Kipindi mafunzo yanaanza ilikuwa tizi la kukimbia umbali mrefu sana,nilikimbia nikachoka sana pumzi ilinizidia nikazima.
Nilivyozinduka nilikula adhabu ya kichurachura na virungu juu.

2-Nilipata rafiki zangu wa Chuga hao ni wakorofi balaa,walipanga kampango tutoroke tukakubaliana.
Mida ya usiku mkali tukaamua kufanya escape from sobibor,hatukufanikiwa tulikamatwa kilichotukuta ni siri yangu.

3-One day tuliingia msituni kwenye mazoezo ya shooting,nikaamua kulala kifudifudi huku naweka target mara mbele yangu yupo mjomba Cobra.Alinipa utamu wa mate yake ya sumu,sikuona chochote wiki nzima nilipatwa na upofu.

4-Siku moja likapigwa Disko la kijeda sasa kuna mjeda mmoja hv akatia aibu.
Alikuwa amebambia mtoto mkali ile mziki kuzimwa jamaa suruali imeloa,tulimcheka sana😂😂😂😂😂hadi alitamani kulia.
Bahati mbaya mimi nna kicheko cha maudhi halafu jamaa alinikariri,alinifanyia visa balaa hadi kunifulisha magwanda ya wakulu daaah.

ILA JESHINI KUZURI SANA ASIKUNANGANYE MTU.
 
Vipi hukuliwa tigo maana naona mengine umeweka kama siri yako, maana hata Roma alipotekwa kilichomkuta huko aliweka siri yake kama wewe mleta ulivyofanya
 
Vipi hukuliwa tigo maana naona mengine umeweka kama siri yako, maana hata Roma alipotekwa kilichomkuta huko aliweka siri yake kama wewe mleta ulivyofanya
Sio tigo mkuu,zilikuwa adhabu kali sana hadi niliona jehanamu.
Nilikuwa nafurahi sehemu moja tu,nayo ya msosi tu kwa sababu nilirudi home nimenenepa licha ya majanga yote.
 
Jeshini ukiwaza kutoroka tu baaaasi unaanza kuteseka. Maana moyo unakuwa umeshatoroka umeacha mwili. Unaambiwa fungua moyo kumve wewe ulifunga ???
Hali niliizoea baada ya miezi miwili,mwezi wa mwisho nilikuwa nusu soldier.
 
Back
Top Bottom