Mimi nachojua, ukiwa na mgogoro wa ardhi na mtu binafai, inawezekena kuzungumza nje ya mahakama. Ni serikali tu ndio huwa inatumia nguvu kubomoa nyumba za watu hata kama kesi ipo mahakamani, au hata kama raia wana haki.
Sasa hao raia wasiwe wabishi, wajaribu kuzungumza nje ya mahakama ili waachiwe nyumba zao.
Hali nayoiona hapa, inawezekena hilo eneo ni la asili la huyo bwana, lakini hakuwepo miaka mingi, hivyo kuna watu ambao ni wenyeji wa huko (majirani) wakalivamia na kuanza labda kulima au shughuli mbalimbali.
Baadae, hao wavamizi wenyeji wakaanza kuuza viwanja kwa wageni. Wageni wakanunua bila kujua.
Mmiliki halali wa asili karudi kaanza kudai eneo. Kilichotakiwa hapa ni wavamizi kukubali matokeo wamlipe huyo jamaa kama kweli eneo ni la asili la huyo jamaa.
Kama eneo ni la asili la huyo bwana, atashinda tu mahakamani! Mana anaweza kuleta mashahidi wazee wa miaka hiyo enzi za kijiji ambapo wanamfahamu hadi babu yao. Je, hao wavamizi wakiulizwa hapa alikuwa analima mzee nani watajua?
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app