Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Hivi inakuwaje watu ambao "profession" yao ni waendesha mnada/wakala wa mahakama, wanapewa kazi kubwa kama hiyo ya kusimamia utekelezaji wa masharti ya leseni za usafirishaji? Au ni kwa sababu Memorandum and Articles of Association inawaruhusu kufanya "kazi nyingine yoyote"? Jamani, tunakwenda wapi? SUMATRA inatupeleka PABAYA sana!
./Mwana wa Haki
swali tangazo la hii tenda lilitolewa lini na SUMATRA na je mbona hatujaambiwa kama sheria za PPRA zilifuatwa na mchakato uliofanywa uliwapitisha akina nani mpaka akapatikana huyu Majembe?
Mkuu wa Usalama barabarani James Kombe akizungumza leo jijini Dar kuhusu utoaji huduma ya usafiri kupitia kampuni ya Majembe Auction Mart.
SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
Yaani Kuanzia Desemba 1, 2009 Kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART imekasimiwa kazi ya kusimamia, kufuatilia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni ya kusafirisha abiria katika jiji la Dar na kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo.
Mbali na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.
surely kwa issue controversial kama UBUNGO BUS stop ilitakiwa SUMATRA waonyeshe due to public interest Business plan yao nzima na malengo gani wanayo katika kufanya kile kituo kiwe user friendly
Ngoja nifafanue Mkuu, ni kwamba Majembe wamepewa uwakala wa kusimamia taratibu za leseni na uratibu wa utekelezaji wa wasafirishaji kwa niaba ya SUMATRA, sio kuendesha kituo cha Ubungo. Hata hivyo SUMATRA walitakiwa kutangaza hiyo tender hilo halina ubishi kama hawakutangaza.
Kituo cha ubungo kiko chini ya City
Tenda waliyopewa niya kukusanya mapato kituo cha mabasi Ubungo au ni kudhibiti madereva wasiofuata sheria??
Sumatra yaipa rungu rasmi kuanzia leo
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), umeipa rungu kampuni ya mnada ya Majembe Auction Mart kusimamia shughuli zote za usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam.
Kampuni hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa inawashughulikia madereva wachafu, wanaokatisha ruti, wanaopandisha nauli wakati wa usiku pamoja na kupita kwenye hifadhi ya barabara.
Aidha, makosa mengine ambayo kampuni hiyo itayashughulikia ni pamoja kukamata magari yaliyotoboka chini, wanayotoa moshi na mambo mengine yote yanayovunja sheria za barabarani.
Uamuzi huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israeli Sekilasa, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Sekilasa alisema kampuni hiyo itafanya kazi sambamba na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa usafiri katika jiji la Dar es Salaam unaboreka.
Alisema ubabaishaji katika shughuli za kuendesha biashara ya daladala umefikia mwisho na kwamba kampuni hiyo imepewa jukumu la kusimamia utendaji wa kila siku wa magari hayo jijini.
Alifafanua kuwa kampuni hiyo itaanza kazi yake leo ambapo wafanyakazi wake watakaa katika maeneo mbalimbali kwenye barabara ili kusimamia mabasi hayo ili yaweze kufanya kazi vizuri.
Sekilasa alisema dereva yeyote ambaye atakutwa na kosa ama gari lake, Majembe Action Mart itamwandikia faini na atatakiwa kuilipa ili aruhusiwe kuingia barabarani tena.
Aliongeza kuwa usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umekuwa na matatizo mengi hasa wakati wa usiku.
Alisema polisi wa usalama barabarani hawatoshi kuwadhibiti madereva wakorofi pamoja na wamiliki wanaokataa kutengeneza magari yao hivyo kuwepo kwa kampuni hiyo kutakomesha matatizo yote.
Sekilasa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wasaidie kufichua utendaji wa kampuni hiyo ambayo mamlaka yake imeingia nayo mkataba wa mwaka mmoja.
Kuhusu malipo kwa kampuni hiyo, alisema itajilipa yenyewe kupitia fedha itakazotoza daladala zenye makosa.
Hata hivyo, alisema kama kampuni hiyo itashindwa kutatua matatizo ya usafiri jijini Dar es Salaam, Sumatra itavunja mkataba huo baada ya mwaka mmoja kumalizika.
Kwa muda mrefu, usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umekuwa na matatizo hasa wakati wa usiku ambapo magari mengi hukataa kufika mwisho wa safari ama kupita njia ambazo haziruhusiwi.
Aidha, wafanyakazi katika magari hayo wamekuwa na lugha za matusi na kuwanyanyasa abiria, mambo ambayo Sekilasa alisema Kampuni ya Majembe itayadhibiti.
CHANZO: NIPASHE