Majembe mapya ya Simba FC

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258

Rais wa Simba, Evans Aveva (kushoto) akimkabidhi Laudit Mavugo (kulia) jezi ya Simba baada ya kusaini
 

Blagnon (katikati) akisaini Mkataba wa Simba SC. Kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Collin Frisch na kushoto Rais wa klabu, Evans Aveva

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIKU moja baada ya kuachiwa kwa dhamana, Rais wa Simba Sc Evans Elieza Aveva jioni ya leo amewasainisha mikataba wachezaji watano wa kigeni.
Aveva alishikiliwa na Polisi, kituo kidogo cha Mabatini, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia juzi hadi jana kwa tuhuma za kuhamishia fedha za klabu katika akaunti yake binafsi.
Baada ya kuachiwa, Aveva leo amewasainisha mabeki Janvier Besala Bokungu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, kiungo Mussa Ndusha kutoka DRC pia na washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Laudit Mavugo wa Burundi.
 

Method Mwanjali (katikati) akisaini Mkataba wa kujiunga na Simba SC leo
 

Bokungu (katikati) akisaini Mkataba wa kuitumikia Simba SC
 

Mussa Ndusha akisaini Mkataba wa Simba
 
Rais wenu mwizi, kila siku walikuwa wakiulizwa hela za Okwi wanajibu hawajapata kumbe alikuwa anazihamishia kwa akina Chung Chang!
 
Hata hizo za MO zitahamishiwa kwa Chung Chang
 
Jamani nitajieni kikosi kizima cha Simba mwaka huu maana naona nyumba ya jirani imeanza kuungua hadi wameitana leo kujiuliza msimu huu watoje
 
....hizo nchi walizotoka zinaisuuza roho yangu; DRC, Zimbabwe, Ivory Coast, Burundi gud, na siku zote Simba ni mafundi wa kusajili, wale jamaa huwa wanasubiri kusikia tunamtaka flani, ndio wanamkimbilia!

Kwa muziki kwa nini jamaa wasiitishe kikao cha dharura leo?!
 
Hizo hela zingetumika kununua mechi kama Yanga. The teh teh
 
Labda majembe auction mart
Kocha - Joseph Omog

Wachezaji wote watakaowatumia
katika msimu wa
2016/2017.

Magolikipa:
1. Vincent De Paul Angban*
2. Peter Manyika
3. Denis Deonis

Beki wa kulia:
4. Hamadi Juma: Coastal
Union
5. Salum Kimenya: Prisons

Beki wa kushoto:
6. Mohamed Hussein
7. Abdi Banda

Mabeki wa kati:
8. Novaty Lufunga
9. Juuko Murushid*
10. Emmanuel Simwanza-
Mwadui FC
11. Janvier Besala Bokungu*

Viungo:
12. Jonas Mkude
13. Awadh Juma
14. Justice Majabvi*
17. Saidi Ndemla
18. Mwinyi Kazimoto
19. Mzamiru Yassin: M.Sugar
20. Mohamed Ibrahim: M.Sugar
21. Mussa Ndusha*

Winga:
22. Peter Mwalyanzi
23. Jamal Mnyate – Mwadui
24. Shiza Kichuya – M. Sugar
25. Hassan Kabunda –
MwaduiFC
Washambuliaji:
26. Ibrahim Hajibu
27. Daniel Lyanga
28. Haji Ugando
29. Mbaraka Yusuf – K.Sugar
30. Laudit Mavugo *
31. Blagnon Goue Frederic *
32. Ame Ali – Azam FC
33. Method Mwanjari*
 
Kila la kheri watani tutakutana uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…