Majeraha kumkosesha mamilioni ya Waarabu Neymar Jr, Al-Hilal kumvunjia mkataba mwezi Januari

Majeraha kumkosesha mamilioni ya Waarabu Neymar Jr, Al-Hilal kumvunjia mkataba mwezi Januari

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Taarifa kutoka tovuti ya michezo ya Brazil, UOL, zinaeleza kuwa klabu ya Saudi Arabia, Al-Hilal, inafikiria kuvunja mkataba wa Neymar Jr. mapema mwezi Januari.
IMG_0574.jpeg

Uamuzi huu unachangiwa na majeraha yanayomkabili Neymar, ambayo yamekuwa yakimzuia kucheza mara kwa mara, akifanikiwa kucheza mechi saba tu tangu alipojiunga na klabu hiyo kwa uhamisho mkubwa kutoka PSG.

Klabu hiyo, ambayo imewekeza kiasi kikubwa kwenye uhamisho na mshahara wa Neymar, sasa inaripotiwa kuwa inatafakari njia za kupunguza hasara zake na kutafuta kipaji kipya, huku ikitazamia kupata mchezaji maarufu kama Cristiano Ronaldo.
 
Nakubaliana nao tena wamechelewa sana
Kupata mchezaji maarufu type ya Ronaldo kwa Sasa ni ngumu ila wamchukue De Brune au Modric maana pale mbele Mitrovic anapiga kazi sana
 
Back
Top Bottom