Majeruhi ya Neymar na Birthday ya dada yake

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
"Nionyeshe marafiki zako nikutajie tabia yako" hiyo ni kauli ya Margareth Thatcher aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Uingereza ambaye wenyewe Waingereza walipenda kumuita "Iron Lady". Alitoa kauli hiyo akimaanisha jinsi marafiki zako wanaweza wakaamua hatima ya tabia na maisha yako kwa ujumla.

Neymar Jr mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya PSG ni mmoja kati ya wachezaji waliotajwa kuwa wangefanya makubwa sana, bahati mbaya kwa wengi Neymar hajafikia matarajio ya wengi licha ya kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2015.

Kuna mkasa mmoja kuhusu Neymar Jr na birthday ya dada yake. Dada yake Neymar anaitwa Rafaella amezaliwa 11/03/1996 huko Brazil. Wawili hawa ni ndugu walioshibana haswa,pengine kwa kuwa wamefatana katika kuzaliwa. Neymar humwambii kitu kuhusu dada yake kama ilivyo kwa dada humwambii kitu kuhusu Neymar.

Sasa kumekuwa na tetesi kuwa kila ifikapo mwezi wa pili (february) Neymar hupata majeraha ambayo huwa yamamweka nje kwa muda fulani mrefu. Tangu Neymar alipoenda Ulaya, kuanzia mwaka 2015 Neymar huwa ni majeruhi katika kipindi hiki cha mwezi February.

Hali hiyo hupelekea kukosekana kwa Neymar katika mechi muhimu za mtoano za klabu bingwa Ulaya. Toka akiwa Barcelona na sasa akiwa PSG.

Kumekuwa na tuhuma za chinichini kuwa Neymar huwa anajiumiza kwa makusudi ili aweze kupata nafasi ya kwenda kusherehekea birthday ya dada yake Rafaella. Na asipofanikiwa kujiumiza basi atafanya makosa ya makusudi uwanjani ili tu afungiwe akose mechi hizo.

Wakati Dunia leo inangojea kwa hamu pambano la PSG dhidi ya Barcelona, kwa Neymar habari ni tofauti, yeye ameumia hatoweza kucheza anaweza akawa jukwaani au tayari anajiandaa kuelekea Brazil kula raha za birthday ya dada yake kipenzi.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo, Neymar anakosekana katika mechi muhimu za Champions League kwasababu ya kujiumiza kwq makusudi au kujipatia kadi za makusudi ili tu apate wasaa wa kutosha wa kwenda kushiriki sherehe ya kuzaliwa ya dada yake, ambapo imefikia mahali watu wamehoji kuwa inawezekana wakawa ni wapenzi.

Huyo ndio Neymar da Silva Santos Jr , ambaye tabia zake za kiswahili zimefanywa ashindwe kuvunja utawala wa Messi na Ronaldo katika zama hizi. Una neno gani kwa huyu mwamba?

Adios Amigo...
 
Neymar atakosa mchezo wa kesho wa PSG Vs Barca kwa kuwa Alhamisi atakuwa Brazil akisherehekea siku ya kuzaliwa ya dada yake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…