Heshima kwako Mzee Serengeti,
Mkuu vipi tena maji siku nne unalia utadhani mtoto kanyimwa maziwa.Wenzako tumeshazoea kukaa bila maji kwa wiki mbili mpaka tatu yakitoka tunapump kwenye tank la lita 3000 mchezo unaendelea.Mwaka 2011 nimeamua kuchimba kisima ili kuepukana na usanii wa AUWSA ambao hawana mkakati wa kupambana na tatizo la maji zaidi ya kununua magari mapya kila mwaka na kutuvalia miyunifomu yao ya rangi ya blue mapauko.
Mamlaka ya maji Arusha inahitaji mabadiliko makubwa sana pengine kukaa sana kwa mkurugenzi wake mhandisi Munisi kunachagia kuliporomosha shirika kwa kiasi kikubwa.