KERO Maji eneo la Tungi, Morogoro bado ni changamoto

KERO Maji eneo la Tungi, Morogoro bado ni changamoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Waziri wa Maji Juma Aweso alivyokuja alibadilisha uongozi kwenye idara ya maji hapa Morogoro na akasema maji yawe yanatoka hadi weekends kwa katikati ya wiki waweke utaratibu kama kutoka yatoke mara mbili au moja na kuanza kutoka nikuanzia asubuhi hadi saa sita usiku, lakini yanakuja kutoka Alhamisi usiku saa Tano muda ambao watu wanataka kupumzika ndio yanatoka ikifika muda Fulani yanakatika yakishakatika hayatoki Tena mpaka Alhamisi ya wiki ijayo usiku.

Tunapata shida kwakweli watu wa Tungi tunateseka sana hiyo weekend ndio kabisa hayatoki hata tone tunaomba mkuu wa mkoa wa Morogoro atusaidie kama hawezi basi Waziri aje maana tunaishi kwa shida na bili zinakuja kubwa maji hatuyaoni mkuu wa mkoa naye yupo kimya.

Mbunge wetu nae hasemi chochote halafu kwenye uchaguzi wanakuja kuomba kura kwetu huku hawafanyi kazi kwakweli hatuwapi tena.

Pia soma
 
Back
Top Bottom